loader
Dstv Habarileo  Mobile
Chapati za sumu zaua wawili, 11 taabani

Chapati za sumu zaua wawili, 11 taabani

WATOTO wawili wamefariki dunia, na wengine 11 wamelazwa katika Hospitali ya Busolwe nchini Uganda baada ya kula chapati zinazodhaniwa kuwa na sumu.

Inaelezwa kuwa wahanga hao ambao ni wa familia moja ya Kalimu Mulongo, mkazi wa kijiji cha Mabale, walipika chapati hizo maarufu kama ‘kabalagala’ kwa kutumia dawa ya kuua wadudu ya mazao ya matikiti maji na mbogamboga.

Watoto hao walitumia dawa hiyo wakijua ni mafuta ya kupikia.

Inaripotiwa kuwa baada ya watoto hao kula chapati hizo walianza kutapita na ndipo walipokimbizwa hospitalini ambapo wawili kati yao; Namusalo ( 5) na Salya, 6, walipoteza maisha.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Bukedi, Ceasar Tusingwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.

Kwa upande wake, daktari waliyewapokea watoto hao, ambaye alitaka jina lake lisitajwe ameeleza kuwa watoto hao walipofikishwa hospitalini hapo walikuwa wanatapika na kuharisha.

“Manusura wa tukio hili wanaendelea vizuri lakini bado afya yao ni dhaifu sana. Tunafanya kila tuwezalo kuokoa maisha yao,” ameeleza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6227bc4918d4e683c592cd29ef98b9d7.PNG

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi