loader
Picha

Simbachawene, Balozi Marekani wajadili uchaguzi mkuu 2020

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amewahakikishia Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk Imni Patterson (pichani), Umoja wa Ulaya (EU), Angola na Kuwait kuwa Tanzania ipo salama na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, utakuwa huru na haki.

Simbachawene alikutana na mabalozi hao, waliofika kwa nyakati tofauti kwenye Ofisi Ndogo za wizara yake jijini Dar es Salaam jana. Aliwaeleza kuwa vyombo vyake, vinaendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao. Kwa kuwa mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, Simbachawene aliwahakikishia mabalozi hao kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki. Pia, alisema wizara yake itawapa ushirikiano mabalozi hao katika masuala mbalimbali ya utendaji kazi.

“Najisikia furaha kwa ujio wenu na karibuni sana wakati wowote, Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa wizara yangu imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio hapa nchini,” alisema Simbachawene kwa mujibu wa taarifa ya wizara yake.

Wakati akizungumza na mabalozi Ikulu jijini Dar es Salaam Januari 21, mwaka huu, Rais John Magufuli aliwaeleza mabalozi hao kuwa Oktoba mwaka huu Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu, ambao ni muhimu kwa nchi yoyote inayofuata misingi ya kidemokrasia kama Tanzania. Rais Magufuli aliwaeleza mabalozi hao kuwa serikali yake imejipanga kuhakikisha kuwa uchaguzi huo, unafanyika katika mazingira ya amani, uhuru na haki.

“Wakati ukifika tutawakaribisha nchi na taasisi mbalimbali kuja kuangalia uchaguzi wetu ili kujionea nchi yetu inavyokomaa katika nyanja ya demokrasia,” alisema Rais Magufuli.

Ikumbukwe kwamba Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, utakuwa Uchaguzi Mkuu wa sita tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini mwaka 1992. Uchaguzi Mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995, ambao Benjamin Mkapa alishinda kiti cha urais. Uliofuata ulifanyika mwaka 2000 ambao alishinda tena. Baada ya hapo ulifanyika tena mwaka 2005, ambao Jakaya Kikwete alishinda na mwaka 2010 alishinda tena.

NAIBU Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi