loader
Picha

Ukimya RT wamshangaza Simbu

MWANARIADHA nyota wa Tanzania, Alphonce Simbu amesema kuwa bado wako katika giza nene kuhusu kambi yao ya Iteni, Kenya kwa ajili ya maandalizi ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

Alisema kuwa hadi sasa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) halijasema lolote kuhusu kambi hiyo, ambayo ilitarajia kuanza mwanzoni mwa mwaka huu kwa ajili ya kuboresha muda kwa wanariadha waliofuzu kwa Olimpiki, ambao ni Simbu na Failuna Abdi. Akizungumza kwa simu kutoka Arusha jana, Simbu alisema anashangazwa na ukimya wa RT kwani hadi sasa hajui lolote lile kuhusu lini kambi hiyo itaanza, licha ya kuandika barua kukubali kwenda kambini na masharti yote yaliyopo.

Alisema kuwa anaendelea na maandalizi ya nguvu kwa ajili ya Lake Biwa Marathoni itakayofanyika Japan Machi 10 na akirudi atakwenda Kenya kambini kwa gharama zake mwenyewe.

“Nimeamua nikirudi kutoka Lake Biwa Marathon nitaenda kupiga kambi Kenya kwa gharama zangu mwenyewe, lengo ni kujiandaa vizuri kwa Olimpiki maana naona RT haieleweki kila siku dana dana, “alisema.

Mwaka jana katika mbio hizo alimaliza wa sita kwa kutumia saa 2:08 na ametamba mwaka huu kufanya vizuri zaidi katika mbio hizo. Hivi karibuni Kaimu Katibu Mkuu wa RT, Ombeni Zavalla alisema hajui lini wachezaji hao watakwenda Kenya katika kambi hiyo na alimtaka mwandishi kumuuliza Makamu wa Kwanza wa Rais Utawala, William Kallaghe, ambaye hakupatikana.

Msemaji wa RT, Tullo Chambo jana alisema maandalizi ya kambi hiyo ya Iteni yanaendelea vizuri na wanariadha hao wanatarajia kuondoka nchini Machi mosi kwenda Kenya.

Alisema Simbu ndiye pekee aliyejibu barua ya RT kukubali kwenda katika kambi hiyo, lakini Failuna hajasema lolote na wamesikia tetesi kuwa huenda asiende Kenya kwa sababu anazozijua yeye.

Alipoulizwa watamchukulia hatua gani za kinidhamu endapo Failuna hatakwenda, Tullo alisema wanasubiri Machi mosi wajue kama atakwenda au la ndio watajua wachukue hatua gani. Alisema kuwa wanariadha hao wakiwa kambini watapewa huduma zote muhimu pamoja na Sh 500,000 kila mwezi kama fedha kwa ajili ya kujikimu wakati wote wa maandalizi yao.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi