loader
Picha

Coastal Union yatuma salamu Yanga

IKIWA imesalia siku moja kabla ya Yanga kuivaa Coastal Union, kocha wa Coastal, Juma Mgunda amesema wamejiandaa kumaliza mchezo huo mapema unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mgunda alisema wamejipanga vizuri na anashukuru vijana wake wanaendelea vizuri wakiwa katika mikakati kamilifu waliyoipanga ili kupata ushindi kama ilivyokuwa katika mechi zao za hivi karibuni.

Kocha huyo alisisitiza kuwa licha ya kupoteza dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi yao ya mwisho, lakini imekuwa sehemu nzuri ya kuangalia mapungufu na walichokosea katika mechi hiyo ili warekebishe baadhi ya mambo na kurejea katika mstari wa ushindi na matokeo mazuri ili wazidi kujiimarisha katika msimamo wa ligi.

Ikumbukwe kuwa timu hizo zitaingia uwanjani zikiwa zimepishana kwa pointi mbili tu. Yanga ipo nafasi ya nne na pointi 40, ikifuatiwa na Coastal katika nafasi ya tano na pointi zake 38, hivyo kila moja kutaka kukaa juu ya mwenzake baada ya dakika 90 za mchezo huo ni wazi itaongeza ugumu na utamu wa mtanange huo.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi