loader
Picha

Wema: Afya yangu haina tatizo

MSANII wa fi lamu nchini, Wema Sepetu amewatoa hofu mashabiki wake kuhusu usalama wa afya yake akidai hana tatizo lolote kama baadhi ya watu wanavyozusha Akizungumza jana alisema mwili aliona nao kwa sasa ndio mwili anaotamani kuwa nao itakuwa rahisi kutimiza malengo yake aliyopanga kufanya kwa mwaka huu.

Wema amelazimika utata uliotawala kwa mashabiki wake waliokuwa wakishangaa hivi karibuni baada ya mwili wake kupungua ghafla tofauti na ilivyokuwa hapo awali. “ Mwili nilionao kwa sasa naupenda zaidi kwani nina kilogram 65, nilitamani kuwa nazo kulingana na urefu wangu, nimekuwa nikipata maswali mengi kwenye mitandano ya kijamii mashabiki wangu wakihoji kuhusu afya yangu, sina tatizo lolote naamini mwili huu utanisaidia kutimiza malengo yangu,” alisema Wema.

Alisema tangu akiwa Miss Tanzania watu walikuwa wanamwona na mwili kama wa sasa hivyo anajitahidi kujitunza abaki na kilo hizo hizo zikiongezeka labda zisizidi Kilogram 70.

Alisema kipindi anawania taji la Miss Tanzania 2006, alikuwa na kilo 59 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita alikuwa na mwili mkubwa kwani alifikisha Kilogram 109 na kuna wakati ulisababisha mipango yake kurudi nyuma. Wema aliyasema hayo jana Dar es Salaam, wakati anaingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Angels inayojihusisha na uuzaji na usambazaji wa nywele bandia za wanawake.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi