loader
Picha

Watendaji watakiwa kuandaa miswada ya sheria kwa Kiswahili

KAMATI ya Sheria na Kanuni ya Baraza la Wawakilishi imewataka watendaji wa wizara na taasisi za serikali wanapotayarisha sheria wahakikishe kwamba zinaandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili ziweze kufahamika na wengi.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Kanuni ya Baraza la Wawakilishi, Rashid Makame Shamsi wakati akiwasilisha maoni ya kamati mbele ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Alisema miswada na sheria 32 imeletwa mbele ya kamati, lakini iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili ni mitano tu ikiwa ni kinyume na kanuni na sheria za Baraza la Wawakilishi.

Alisema lengo la miswada hiyo kabla ya kuletwa inatakiwa kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kuisoma na kutoa maoni. Alisema miswada na kanuni za Baraza la Kiswahili kuletwa mbele ya baraza ikiwa imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza ni kwenda kinyume na katiba namba 87 pamoja na kanuni za Baraza namba 25.

“Spika, miswada mingi ya sheria na kanuni za baraza inaandikwa kwa Kiingereza, lugha ambayo sio rasmi kwa matumizi ya Baraza la Wawakilishi,” alisema.

Aidha alisisitiza na kuzitaka wizara kabla ya kuleta mswada na kusomwa mbele ya Baraza la Wawakilishi kuhakikisha imewashirikisha wananchi. Alisema utafiti umefanywa na kubaini sheria nyingi zinazopitishwa Baraza la Wawakilishi wananchi hawazijui wakati ndio walengwa wakubwa.

“Sheria zote kabla ya kuletwa mbele ya Baraza la Wawakilishi kwanza tuwashirikishe wadau kwa kutoa maoni yao. Sheria hizo walengwa na watekelezaji wakubwa ni wananchi,” alisema.

MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi