loader
Dstv Habarileo  Mobile
Korea Kusini yachukua tahadhari ya corona

Korea Kusini yachukua tahadhari ya corona

KOREA Kusini imechukua hatua kudhibiti kusambaa virusi vya corona kufuatia ongezeko la kasi la maambukizi kwa siku ya pili sasa. Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Chung Sye-Kyun alitangaza hali ya dharura na tahadhari juzi.

Miji ya Kusini mwa nchi, Daegu na Cheongdo imetangazwa ukanda maalumu wa matibabu. Mitaa ya Daegu imekimbiwa na kutelekezwa. Nchi hiyo pia imefungia majeshi yake baada ya baadhi ya wanajeshi wake kupimwa na kugundulika wameathirika na virusi vya corona.

Waamini 9,000 wa madhehebu mbalimbali ya dini wametakiwa kutokuwa na mikusanyiko na kujiwekea karantini binafsi kwa kuwa ni eneo linaloweza kushambuliwa zaidi na virusi hivyo. Jana, Ijumaa, mamlaka za afya za nchi hiyo zilitoa taarifa ya maambukizi mapya 52 baada ya watu 53 kuthibitishwa kuambukizwa juzi.

Korea Kusini ina waathirika 156, kati yao idadi kubwa ya waathirika wa kutoka nje ya China. Mamlaka zilitangaza kifo cha kwanza nchini humo mji wa Cheongdo, mapema wiki hii.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5a022cb9e59d55f218334e762e6b6bc9.jpg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: CHEONGDO, South Korea

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi