loader
Picha

Mtatiro ataka vyama vya akiba, mikopo kuzingatia sheria

MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro amevitaka vyama vya akiba na mikopo kuzingatia taratibu na sheria na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kuepusha vyama kufa.

Mtatiro alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati alipofungua mafunzo ya siku tatu ya vyama vya akiba na mikopo yaliyoandaliwa na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Ruvuma.

Mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), Chuo cha Ushirika Moshi na maofisa ushirika wa wilaya ya Tunduru.

Mtatiro aliwaonya viongozi hao kuacha mchezo mchafu na vitendo visivyokubalika na kuwataka wana ushirika kuwa ma msimamo wa kujali wakulima na ukuaji wa vyama vya ushirika.

Aidha aliwakumbusha viongozi wa ushirika serikali iko macho na itahakikisha wale wote wanaotaka kujaribu kuyumbisha ushirika katika chaguzi zinazoendelea watachukuliwa hatua za kisheria.

Mtatiro aliwataka wanaushirika kuuchukulia ushirika kama sekta muhimu na yenye tija akitolea mfano Tunduru msimu wa mwaka 2018/2019 wakulima walipata Sh bilioni 61 zao la korosho.

Mtatiro alisema katika msimu wa mwaka 2019/2020, wakulima wa Wilaya ya Tunduru wamepata kiasi cha Sh bilioni 67 huku wakitarajia kupata zaidi ya Sh bilioni tano kutokana na zao la ufuta.

Alisema fedha zote zinapitia vyama vya msingi vya ushirika. Aliwataka wadau wa vyama hivyo kuwachagua viongozi wenye uwezo na wanaolinda na kutetea maslahi na fedha za wakulima.

MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Tunduru

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi