loader
Picha

NGORONGORO RACE 2020 Maandalizi yake usipime

MAANDALIZI ya Ngorongoro Race 2020 yanaendelea kwa kasi, ambapo wanariadha wametakiwa kujiandaa vizuri ili kuhakikisha wanatamba katika mbio hizo zitakazofanyika Aprili 19 mwaka huu.

Meta Petro, ambaye ndiye mratibu wa mbio hizo ambazo hufanyika kila mwaka, alitoa wito kwa wanariadha kujiandikisha na kuanza maandalizi mapema ili kufanya vizuri katika mbio hizo.

Mwaka jana mbio hizo zilishirikisha karibu wakimbia 1,000 wa mbio za kilometa 21, tano na 2.5, ambazo ni mahsusi kwa watoto wadogo. Msimu uliopita, ambao Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala ndiye alikuwa mgeni rasmi, pia alikimbia na kumaliza mbio za kilometa 21, ambazo zilianzia katika Lango Kuu la kuingia na kutokea katika mbuga za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

MAANDALIIZI MAPEMA

Petro aliwataka wanariadha wenye nia ya kushiriki katika mbio za kilometa 21, tano na zile za watoto za 2.5, kuanza maandalizi mapema ili kuhakikisha wanakomba zawadi zote mwaka huu.

Anasema kuwa zawadi za mwaka huu zitatangazwa baadae, lakini tayari wadhamini wakuu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ndio wataendelea kuwa wadhamini wakuu, huku Bonite Bottlers nao wakikubali kuendelea kuwa miongoni mwa wadhamini.

Anasema anazipongeza NCAA na Bonite kwa kukubali kuendelea kuwa nao mwaka huu, ambapo alizitaka taasisi zingine nazo kujitokeza kudhamini mbio hizo za aina yake, ambazo zinapiga vita uwindaji haramu. KAULI MBIU 2020 Petro anasema kuwa mwaka huu wa 2020 wataendelea na kauli mbiu yao ya Kupiga Vita Uwindaji Haramu, ambao umekuwa ukiwaua wanyama, ambao wamekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa utalii.

Anasema mauaji hayo ya wanyama yamekuwa yakileta hasara kwa taifa kwa kuwaua ovyo wanyama, hivyo amewataka watu kujitokeza kwa wingi katika mbio hizo ili kupiga vita vitendo hivyo vya kinyama. Anasema kuwa wataendelea kutangaza vita hivyo dhidi ya wauaji hao wa wanyama pori, ambao wamekuwa wakiingiza fedha nyingi kwa watalii kuja kuwaona. Anasema matarajio yao mwaka huu watajitokeze wanariadha wengi kuanzia mbio za kiometa 21, tano na zile za watoto za kilometa 2.5, ambazo mwaka jana zilitia fora kwa kuwa na washiriki wengi.

KUIBUA VIPAJI

Pia mbio hizo zina lengo la kuinua vipaji kwa vijana na watoto wadogo. Anasema kuwa wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha vipaji vya watoto kutoka ukanda huo wa Karatu, Babati, Ngorongoro na maeneo ya jirani vinaibuliwa na kuendelezwa ili kuhakikisha mchezo huo unakuwa zaidi na zaidi.

MBIO ZA MWAKA JANA

Baada ya kutawaliwa kwa muda mrefu na Watanzania, mbio za mwaka jana zilitawaliwa na Wakenya, ambao walichukua nafasi zote za juu na kuondoka na zawadi nono. Mshindi wa kwanza kwa wanaume katika mbio hizo za mwaka jana alikuwa Mkenya, Joseph Mbata kwa kutumia saa 1:04.54.12 akifuatiwa na Mkenya mwenzake, Benard Mussa aliyetumia muda wa saa 1:05:09.59 Wakati Mtanzania wa kwanza ni Pascal Mombo aliyeshika nafasi ya tatu kwa saa 1:06:05.71. Kwa upande wa wanawake, Wakenya walkiendelea kutamba baada ya mwanariadha wake, Monica Cheruto kumaliza wa kwanza.

Huku Mtanzania Failuna Abdul akimaliza wa pili. Failuna alikuwa miongoni mwa wanariadha wa Tanzania walioshiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Gold Coast, Australia iliyomalizika Aprili 15 mwaka jana, lakini hakufanya vizuri katika mbio za meta 5,000 na 10,000.

Kwa upande wa kilometa tano, mkimbiaji wa siku nyingi wa Tanzania Mary Naali (Arusha) alimaliza wa kwanza kwa upande wa wanawake alipotumia dakika 17:40.65 wakati mshindi wa pili alikuwa Rozalia Fabiani alitumia dakika 17:55.56 (JKT) wakati watatu ni Anastazia Mkama wa Mara alitumia dakika 18:01.40 .

Katika mbio za kilometa tano kwa wanaume mshindi wa kwanza ni Elibariki Buko wa JKT alitumia dakika 14:14.81 huku mshindi wa pili ni Marco Sylvester wa JKT alitumia dakika 14:14,86. Kwa mwaka juzi Watanzania walitamba katika kilometa 21 kwa wanaume na

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi