loader
Picha

Hapi ataka wafungwa wachimbe mitaro

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ametoa wito kwa Jeshi la Magereza Iringa kuruhusu wafungwa wake kuchimba mitaro ya miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Iruwasa) ili kupunguza deni la zaidi ya Sh milioni 300 wanazodaiwa na mamlaka hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Iruwasa, Gilbert Kayange kwa mkuu wa mkoa huyo ililitaja jeshi la Magereza kama moja ya taasisi za serikali ambazo ni wadaiwa sugu wa mamlaka hiyo.

Hapi alitembelea mamlaka hiyo hivi karibuni ikiwa ni siku ya kwanza ya awamu ya pili ya ziara yake ya ujenzi wa Iringa Mpya inayolenga kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo na kupokea changamoto zinazowakabili wananchi na taasisi mbalimbali.

Kayange alisema mamlaka yao inazidai taasisi mbalimbali za umma na binafsi, na moja ya taasisi hizo ni gereza la mkoa wa Iringa linalodaiwa kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho kama kingelipwa kwa wakati kingeweza kuboresha shughuli zao mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa alisema deni wanalodaiwa gereza hilo ni kubwa na akatoa wito kuanza kulipunguza ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuruhusu wafungwa wake watumike kufanya shughuli za mamlaka hiyo ili fedha watakazotakiwa kulipwa zikatwe katika deni hilo. Hapi alisema kujitegemea ni muhimu kukaenda sambamba na kulipa madeni ya gereza hilo.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeshauri ujenzi wa ...

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi