loader
Picha

Yanga yaifuata Simba FA

YANGA ya Dar es Salaam jana iliungana na Simba, Sahare All Stars, Ndanda na Namungo FC kucheza robo fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuifunga Gwambina kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Bao hilo pekee katika mchezo huo liliwekwa kimiani na Haruna Niyonzima katika dakika ya 45 baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 lililojaa kimiani akimalizia mpira uliokolewa na mabeki wa Gwambina inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza (FDL).

Dakika ya 80, Morrison aliikosesha Yanga bao la pili baada ya kubaki yeye na kipa wa Gwambina, ambaye aliupangua mpira huo.

Katika kipindi cha kwanza, Gwambina walionekana kungangamala na kujaribu kulishambulia lango la wapinzani wao hao kabla ya kufungwa bao hilo, ambalo limeivusha Yanga kutoka katika hatua ya 16 bora.

Katika mchezo mwingine jana, mabingwa watetezi wa kombe hilo, Azam FC ilitinga robo fainali kwa penalti 5-4 dhidi ya Ihefu FC katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.

Bingwa wa mashindano hayo ataiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao. Katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imekuwa ikisuasua baada ya kupata sare nne mfululizo, hivyo ushindi huo wa leo utarejesha matumaini kwa mashabiki wake, ambao wameanza kukata tamaa ya ubingwa wa VPL.

Sahare All Stars wenyewe walitinga robo fainali baada ya kuifunga Panama FC kwa mabao 5-2 Jijini Dar es Salaam, huku Namungo ikiichapa Mbeya City kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Ndanda FC wenyewe walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kitayosa FC katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kagera Sugar imetinga hatua ya robo fainali baada ya kuifunga KMC kwa penalti 2-0 baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana 1-1 katika muda wa dakika 90 za mchezo huo kwenye Uwanja wa Kaitaba, Alliance nao walifuzu kwa penalti 5-3 dhidi ya JKT Tanzania, baada ya kumaliza 1-1 katika dakika 90.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi