loader
Picha

Benki yadhamini Bima Marathoni kwa milioni 35/-

BENKI ya NMB imetoa kiasi cha Sh milioni 35 kwa ajili ya kudhamini Bima Marathoni itakayofanyika Machi 28 Mlimani City, Dar es Salaam. Jumla ya wanariadha 4,000 wa rika tofauti wanatarajiwa kushiriki mbio hizo, ambazo hufanyika kila mwaka nchini.

Meneja Mwandamizi wa NMB jana, Martine Massawe alisema wanajisikia furaha kuwa wadhamini wakuu wa mbio hizo kwani moja ya mipango yao ni kuendeleza michezo nchini na kuboresha afya za Watanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa African Banking Summit, ambao ndio waandaji wa mbio hizo, Baraka Mtavangu alishuruku uongozi wa NMB kwa udhamini huo na kusema watajitahidi kuhakikisha wanatumia vyema ili kuwashawishi watu kutumia huduma za benki hiyo.

“Bima Marathoni itakuwa ikiitwa NMB Bima Marathoni, kwa sababu ndio mdhamini mkuu na tunajivunia tukiamini yatafanyika kwa ubora wa hali ya juu tofauti na miaka ya nyuma,” alisema Mtuvanga.

Mtavangu alisema mbio hizo zitakuwa za kilometa 21 na 10 na watoto wadogo na washiriki watalipa kiingilio cha Sh 20,000 na watoto wadogo ni Sh 15,000.

Pia Mtavangu alisema zawadi ya mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 21 ni Sh milioni 1 wakati mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 10 akijinyakulia Sh 700,000 wakati mshindi wa kwanza kwa mbio za watoto ataondoka na medali.

Mtavangu alisema maandalizi yanakwenda vizuri na mbio hizo zinatarajia kuanzia Mlimani City, na njia zitakazotumika zitatangazwa baadae na washiriki katika mbio hizo ni raia wa Tanzania na wageni wanaoishi hapa nchini.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi