loader
Picha

Klabu zatakiwa kuwasilisha taarifa za usajili

MSAJILI msaidizi wa vyama na klabu wa jiji la Arusha, Benson Maneno, amezitaka klabu zote zilizosajiliwa katika jiji hilo kuwasilisha taarifa za usajili kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha pamoja kitakachofanyika mwezi ujao.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa mwenendo usioridhisha wa uchaguzi wa chama cha soka Wilaya Arusha Mjini (ADFA), ambacho mchakato wake ulianza Juni 2019 lakini haukukamilika kutokana na katiba kuwa na mapungufu na kuagiza mkutano wa dharura lakini hawakuitisha.

“Arusha Mjini kuna vyama na klabu 390 hivyo natarajia wote watasilisha taarifa zao ambazo ni namba ya cheti cha usajili ,katiba zao orodha ya viongozi kwa ajili ya kufanya mkutano wa pamoja ili kuanza mchakato mzima wa uchaguzi. Zoezi hili litafanyika kuanzia Februari 24 hadi Machi 2 katika ofisi zetu zilizopo halmashauri ya jiji,” alisema Maneno.

Maneno amesema lengo ni kuona wilaya ya Arusha mjini inakuwa chama kilicho bora na hai kikiwa na timu hai kwa sababu hakuna uongozi imara wa chama kuna timu kama Madini ambayo nayo ilipotea, AFC na nyinginezo zimekuwa zikiyumba sababu hakuna uongozi imara.

“Arusha ni miongoni mwa jiji imara Tanzania hatuwezi kuwa na viongozi legelege kwenye chama cha soka lazima kuwepo na uhai ili timu zisimame na sisi serikali tumeamua kuingilia kati ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda,” amesema Maneno.

Pia amesema wajumbe wa mkutano mkuu ndio wataamua kwani baada ya kuunda kamati zao za uchaguzi serikali inawatengenezea njia kusimamia uchaguzi na utasimamiwa na kamati ya uchaguzi kwa mujibu wa katiba yao.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Yasinta Amos, Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi