loader
Picha

Zanzibar kuvuna rasilimali baharini

SERIKALI ya Zanzibar imesema Mpango wa Maendeleo na Dira ya Taifa 2050, utajikita zaidi katika ‘uchumi wa bluu’ wa kuvuna rasilimali zilizomo baharini ikiwamo uvuvi wa bahari kuu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa, wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Zanzibar ya mwaka wa fedha 2020/2023 katika Baraza la Wawakilishi.

Balozi Abdiwawa amesema, ‘uchumi wa bluu’ unaotokana na kuvuna rasilimali za baharini, ni moja ya mikakati ya Zanzibar kuingia katika uvuvi wa bahari kuu.

Alisema moja ya juhudi zilizochukuliwa na serikali ni kuanzisha Taasisi ya Uvuvi Zanzibar (Zafico), ambayo malengo yake ni kuelekea katika uvuvi wa bahari kuu.

Alisema utafiti uliofanywa, umebaini kwamba Zanzibar haijatumia vizuri eneo la bahari kuu kwa ajili ya kuvuna rasilimali za samaki pamoja na nishati ya mafuta.

‘’Zanzibar haijalitumia eneo la uvuvi wa bahari kuu kwa ajili ya kuvua samaki wakubwa ikiwamo jodari, wapo wageni hujipenyeza na kuvua samaki katika eneo letu kinyume cha sheria,’’ alisema.

Balozi Ramia aMesema serikali ya Zanzibar inatarajia kununua meli nne kwa ajili ya kuvua katika maeneo ya bahari kuu na kuvuna rasilimali zilizopo.

‘’Tumenunua meli kubwa ya uvuvi na tunatarajia kununua nyingine kwa ajili ya shughuli za uvuvi wa bahari kuu ili kuweza kuvuna utajiri uliopo kwa maslahi ya wananchi wetu,’’ alisema.

Waziri wa Kilimo, Maliasili Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri, alisema tayari Zafico kwa kutumia meli yake imeanza shughuli za uvuvi wa bahari kuu katika ukanda wa bahari ya Zanzibar.

MKURUGENZI wa Wakala wa Misitu Tanzania, TFS, Santos Salayo ameonya ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi