loader
Picha

Wabunge Kigoma wataka uwazi miradi UN

WABUNGE wa Mkoa Kigoma wametaka uwepo uwazi wa taarifa za utekelezaji na taarifa za fedha za miradi iliyo chini ya taasisi za Umoja wa Mataifa (UN) kwa kuwa taasisi na mashirika hayo wanatekeleza miradi mingi inayotumia kiasi kikubwa cha fedha lakini upatikanaji wa taarifa za miradi hiyo ni mgumu.

Mwito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Kigoma, Daniel Nsanzugwanko mjini Kigoma.

Amesema hayo alipoongoza timu ya wabunge wa mkoa huo na Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya mkoa huo kukagua miradi inayotekelezwa chini ya Mpango wa Pamoja Kigoma (KJP) inayotekelezwa na mashirika 16 ya UN nchini.

Nsanzugwanko amesema ametembea na kuona miradi mikubwa na yenye manufaa makubwa kwa wananchi lakini baadhi ya miradi hakuwa anaijua na taarifa zake hazikuwa zikipatikana.

Alisema lazima miradi hiyo taarifa zake ziwe zinatolewa kwenye vikao mbalimbali vya kiserikali kama ambavyo zinatolewa taarifa za miradi inayotekelezwa kwa fedha za serikali.

Pia alisema iko haja taarifa hizo zipatikane kwa wakurugenzi ili viongozi mbalimbali wanaotaka taarifa hizo waweze kuzipata kwa urahisi zaidi. Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Augustino Vuma naye alisema ipo miradi mikubwa yenye manufaa makubwa kwao lakini baadhi yake h hawakuwa wanaijua na ziara hiyo imewafungua macho na kuona mabilioni ya fedha za UN zinazotumika kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

Wabunge hao wameridhishwa na utekelezaji miradi chini ya KJP wakisema miradi hiyo imeleta faida, mabadiliko makubwa kwa jamii. Waliitaja miradi husika ni ya sekta za elimu, maji, uwezeshaji, ujenzi wa masoko ya mpakani na uanzishaji shughuli za wananchi kiuchumi.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mratibu wa miradi ya KJP, Evance Siangicha alisema zaidi ya Sh bilioni 100 zinatarajia kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali chini ya mpango huo na miradi hiyo imelenga kuleta faida na mabadiliko makubwa kwa jamii.

Amesema miradi hiyo imeanzishwa kutekeleza mpango wa kuanzisha miradi maeneo yaliyoathiriwa na wakimbizi Kigoma kufuatia mkoa huo kuhifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wa nchi za maziwa makuu muda mrefu.

Amesema utekelezaji wa miradi yote imekuwa ikitolewa taarifa kwenye vikao mbalimbali ikiwemo kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa. Vikao vingine ni vya halmashauri zas wilaya na Manispaa.

Alisema kwa sasa wapo wawakilishi wa programu hiyo katika sekretarieti ya mkoa na kwenye halmashauri ambao moja ya kazi zao ni kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo katika vikao mbalimbali maeneo yao.

MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi