loader
Picha

Shinyanga wataka soko la mchele EAC

WAFANYABIASHARA wa mchele mkoani hapa wameomba kuwepo kwa soko la pamoja Afrika Mashariki la uuzaji wa mchele kwa kuwa Rwanda na Uganda wamekuwa wakinunua mchele wa daraja la kwanza nchini na kuufungasha upya wakionesha unatoka kwenye nchi zao.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mchele Kagongwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Marando Dili ametoa kilio hicho leo wakati wa kikao cha mashauriano ya wafanyabiashara mkoani Shinyanga .

Dili amesema madalali wa kutoka Rwanda na Uganda wamekuwa wakiingia katika mikoa ya Shinyanga , Morogoro na Mbeya kuchukua mchele bila kizuizi chochote.

Hali hiyo imewafanya Watanzania kushindwa kuingia kwenye soko la ushindani wanapoufikisha mpakani mchele wa Tanzania kwani hawaruhusiwi kuingia nchi hizo na mchele.

Dili alisema kuwa wafanyabiashara wa Tanzania wanakosa ajira kutokana na madalali waliopo mpakani eneo la Maji moto Rwanda wamekuwa wakifanya mchezo huo.

"Mfuko una TBS kutoka Tanzania unapofika huko wanabadilisha mifuko yenye nembo zao, kikawaida walitakiwa kuuza hivyo hivyo ili ufahamike umetoka Tanzania. Kufanya hivyo ni kuwakosesha masoko ya kuweza kutambulika uking'ang'ania utasota mwezi mzima unauza lakini ukiwapa madalali wao unauza siku moja," alisema.

Mbunge wa jimbo la Kahama mjini, Jumanne Kishimba alisema kuwa kweli hayo yanafanyika ya kutotangaza mchele wenye daraja la kwanza kutoka wilayani Kahama.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba amesema bidhaa ikiwa na jina analotaka mteja ni kufanya makubaliano, haina shida kwani bidhaa lazima ionekane inatoka wapi hivyo wafanyabiashara hao wanafanya makosa kubadili nembo.

"Hii haingii akilini badala ya kutuongezea wateja inatupunguzia ilikwishawahi siku moja kutukosesha soko la chai uarabuni kwani ilikuwa mifuko imeandikwa Kiswahili na huko wakitaka iandikwe kiarabu, ndivyo hata soko la Afrika Mashariki linatakiwa bidhaa ionekane inatoka wapi sio kujinufaisha wao na kutupungiza mapato yetu,"alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack alisema katika operesheni ya kukagua vifungashio wilayani Kahama walikuta maghala yaliyokuwa na mifuko yenye nembo ya Uganda.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu alisema wafanyabiashara wa Tanzania wamekosa vibali vya kuingiza bidhaa nchini humo hivyo bado elimu ya soko la pamoja inahitajika.

Alisema taarifa zilizopo wanyarwanda wananunua mpunga na kutumia mashine za hapa nchini kukoboa na kusafirisha kwao.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji alisema “Ukitaka kubadili nembo ina gharama yake, kufanya kinyemela huko ni kuiba lakini hili linazungumzika, linakwenda kwenye mchakato litapelekwa kwenye mkutano wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC)”.

MKURUGENZI wa Wakala wa Misitu Tanzania, TFS, Santos Salayo ameonya ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi