loader
Picha

Skauti kukabili rushwa ya ngono shuleni, vyuoni

MKUU wa Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza amesema Chama cha Skauti kimejipanga kupambana na rushwa ya ngono kuanzia ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vikuu.

Mahiza ameyasema hayo jijini Dodoma na kuongeza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kuingia makubaliano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya kutoa elimu ya kupambana na vitendo vya rushwa kwa wanafunzi.

Amesema kutokana na makubaliano hayo, Chama cha Skauti kimejipanga kuanza kutoa elimu kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu ili kukabiliana na vitendo vya rushwa ikiwemo ya ngono inayowatesa wanafunzi wengi.

Lengo la kufanya hivyo ni kutokomeza rushwa katika maeneo mbalimbali na kusisitiza kuwa rushwa ya ngono ni tatizo kubwa ambalo linatesa jamii hususani vijana wadogo ambao ni nguvu kazi ya kesho ya Taifa.

"Tumeamua kushirikiana na Takukuru ili kuhakikisha wanatokomeza kabisa rushwa hapa nchini." Mahiza alisema hivi sasa ana kazi kubwa ya kuingia katika shule hadi vyuo ili kutoa elimu kwa vijana.

"Hivi sasa kuna vuguvugu la siasa, pia sisi skauti tutapambana ili kutokomeza rushwa na niwaase wanasiasa hakuna sababu ya kukashfiana, kinachotakiwa ni kuandaa mikakati ili kuwashawishi wananchi wakuchague," alisema.

Alisema rushwa ya ngono inatesa na kusababisha vijana wengine kupata ugonjwa wa Ukimwi.

"Tutasaidiana na klabu za wapinga rushwa ili kuwaokoa wanafunzi, na wahadhiri wa vyuo waache tabia ya kuwarubuni wanafunzi ambao wanategemewa na taifa la kesho."

Aidha, Mahiza alisema Chama cha Skauti kinatarajia kuzindua kongamano la elimu ambalo litakuwa kama kichochezi cha utoaji elimu elekezi kwa jamii.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo alisema bado kuna mwamko mdogo wa wananchi wa kutoa taarifa za rushwa hali inayosababisha taasisi hiyo kufanya kazi kwa shida.

MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi