loader
Picha

Meneja Tanroads apewa siku 2 maeneo korofi

MENEJA wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mbeya, amepewa siku mbili kuhakikisha anakarabati maeneo korofi yaliyoathiriwa na mvua katika barabara ya Isyonje- Makete (Km 96.4) ambayo inaunganisha mkoa wa Mbeya na Njombe.

Katika taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inaonesha kwamba Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga ametoa siku mbili baada ya kutembelea barabara hiyo na kuona athari za mvua katika miundombinu katika eneo la Igoma, mkoani Mbeya.

Mwakalinga akiwa katika kijiji cha Igoma alisema barabara hiyo ni muhimu kwani ni kiungo cha mawasiliano kati ya mikoa hiyo miwili ya Njombe na Mbeya.

"Meneja hakikisha barabara hii inapitika ifikapo kesho, kusanya wataalamu wako wote waliopo katika mkoa wako, mje hapa kufanya kazi ili kuhakikisha barabara hii inarudi katika hali yake ya awali,"amesema.

Amesema licha ya mvua kuendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo lakini bado wananchi wanahitaji hali nzuri ya barabara ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji wa abiria na mazao kutoka sehemu mbalimbali.

Mwakalinga alisema ameamua kufanya ziara hiyo ili kubaini athari za mvua katika miundombinu ya barabara na kutatua changamoto zake pamoja na kuangalia maendeleo ya miundombinu hiyo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuzipa kipaumbele katika kuzitengea fedha barabara zote zenye changamoto kwenye bajeti ijayo.

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Mbeya, Eliazary Rweikiza, alimhakikishia Katibu Mkuu huyo kuwa atakarabati kwa wakati barabara hiyo ili kupitika majira yote ya mwaka.

Pia alisema tayari mkandarasi ameshaaanza kurekebisha sehemu zilizoharibika na kwamba ndani ya siku mbili kazi zote zitakuwa zimekamilika na barabara kupitika vizuri.

MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi