loader
Picha

Corona kuathiri Mwenge Olimpiki

KUENEA kwa virusi vya corona kunawafanya waandaaji wa Michezo ya 32 ya Olimpiki, Tokyo 2020 kufikiria kufuta sherehe za mbio za Mwenge wa Olimpiki, kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu, Toshirō Mutō.

Vyombo vya habari vya Japan vimemkariri Muto akisema kuwa, mbio hizo ni tukio muhimu kwa ajili ya kuhamasisha michezo ya olimpiki, lakini zinaweza kupunguzwa kasi yake, ikiwa ni sehemu ya kuzuia kuenea kwa virusi hivyo hatari.

Hata hivyo, Muto alisema mbio za mwenge huo ambazo zinatarajiwa kuanza huko Fukushima Prefecture Maon Machi 29, hazitafutwa licha ya kulipuka kwa janga la virusi vya corona.

Kupunguza ukubwa wa sherehe za kuanza na kumaliza mbio hizo ni sehemu ya hatua zitakazochukuliwa katika Olimpiki ya 2020 Tokyo, ikihofiwa kuenea kwa virusi hivyo, ambavyo tayari vimeshaua watu 2,770 na kuwaambukiza zaidi ya 81,000 duniani kote.

"Kuwaleta watazamaji katika eneo moja kwa idadi kubwa ni hatari kubwa kwa maambukizi haya," alisema Mutō, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kyodo.

"Kupunguza shamrashamra ni sehemu ya njia tunazozifikiria kuzifanya ili kupunguza tatizo hilo."

Virusi vya corona vimekuwa tishio kubwa kwa mashindano ya kufuzu kwa Olimpiki, huku kukiwa na ushauri kuwa michezo hiyo mikubwa zaidi duniani iahirishwe au ifutwe kabisa, wakati waandaaji wake ambao ni Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) wakitupilia mbali wazo hilo.

Richard Pound, ambaye ni mjumbe mzito wa IOC, aliliambia Shirika la Habari la Associated Press (AP) kuwa, hawajafanya maamuzi yoyote hadi mwezi Mei.

Alisema michezo ya Olimpiki inaweza kufutwa endapo virusi hivyo, ambavyo vimepewa jina la COVID-19 na Shirika la Afya Dunia, havitadhibitiwa hadi wakati huo.

Kuenea kwa virusi hivyo nchini Japan kumezua minong’ono kuwa, huenda hilo likalazimisha kufutwa au kuahirishwa kwa michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

Wataalamu wamesema michezo hiyo haiwezi kufutwa au kuahirishwa kwa sababu kutatokea hasara kubwa kwa waandaaji, pia kwa wadhamini, watangazaji na wadau wengine.

Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 inatarajia kuanza Julai 24 hadi Agosti 25 na inatarajia kuvutia mamilioni ya watazamaji ambao watakwenda Japan kushuhudia wachezaji zaidi ya 11,000 kutoka mataifa 200 wakichuana.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: TOKYO, Japan

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi