loader
Picha

Mchezaji Cameroon asaidia waathirika wa corona

MSHAMBULIAJI wa Cameroon, Christian Bassogog, ametangaza kuwa, atachangia Dola za Marekani 16,000 (sawa na Sh milioni 37), kwa ajili ya wanafunzi wa Cameroon wanaoishi nchini China katika maeneo yaliyoathirika na corona.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye alijiunga na Ligi Kuu ya China katika klabu ya Henan Jianye mwaka 2017, kwa sasa yuko Yaounde, Cameroon baada ya soka nchini China kusimamishwa kwa sababu ya virusi vya corona.

Ubalozi wa Cameroon nchini China umesema kuna karibu wanafunzi 300 wa Cameroon nchini humo, ambao wanaishi katika Jimbo la Hubei na karibu wanafunzi 200 kwa sasa wako katika jiji la Wuhan ambalo liko chini ya uangalizi tangu Januari 23.

"China ni sehemu maalum katika moyo wangu, ambako ninacheza soka,"alisema Bassogog baada ya mkutano na msafara wa Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa wa Cameroon anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Madola.

"Fedha hizi zina lengo la kuwasaidia wananchi wa Wacameroon wanaoishi China hasa wanafunzi waliopo katika maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo.”

"Muhimu kuwa tumekuja pamoja katika vipindi hivyo na kuonesha msaada kama huo kwa wahitaji. Tunataka Wacameroon duniani kote wajitokeze kusaidia na sio watu wao wa Cameroon tu, bali pia taifa la China kwa ujumla.”

Msaada wake huo umekuja baada ya Rais wa taifa hilo la Magharibi ya Afrika, Paul Biya, kuamuru kiasi cha Dola za Marekani 82000 (sawa na Sh 108,403,600) kupelekwa katika ubalozi wao Beijing, ili kusaidia Wacameroon wanaishi katika maeneo yaliyoathirika.

Bassogog, ambaye amejulikana baada ya kuwa mchezaji bora wa mashindano ya mataifa ya Afrika, Afcon 2017, wakati Cameroon ilipotwaa taji hilo, amesema mchango wake huo utaweza kuwaibua wachezaji wengi wa Cameroon kusaidia matatizo ya dawa nchini humo.

Mapema mwezi huu, mwanafunzi wa Cameroon, Kem Senou Pavel Daryl, alibainika kuathirika na ugonjwa huo huko Zhengzhou, katika jimbo la Henan.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: YAOUNDE, Cameroon

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi