loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samatta kuonana na Guardiola Wembley

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta leo atakuwa na kazi kubwa wakati timu yake ya Aston Villa itakapokuwa ikiwakabili Manchester City kwenye fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Carabao Cup.

Samatta aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni amekuwa aking’ara na baba yake amesafiri kwenda Uingereza kushuhudia mtanange huo mkali. Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja mkubwa wa England unaomilikiwa na chama cha soka cha taifa hilo, Wembley.

Tayari Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema wana kiu ya vikombe wakati huu ambapo wanaelekea kupokonywa ubingwa wa ligi ya England kutokana na kuachwa mbali mno na vinara wa ligi hiyo Liverpool.

Aston Villa wanaingia wakiwa hawapewi nafasi kubwa, lakini Samata na Jack Grealish wanaweza kufanya maajabu kwenye safu ya ushambuliaji na kumaliza miaka miwili ya utawala wa Man City kuchukua kombe hilo. Guardiola haibezi Villa na anasema hawezi kuwa na uhakika wa kushinda kwa sababu wapinzani wao nao wamejipanga kushinda.

“Kamwe huwezi kusema unakwenda kushinda. Hiyo ni kukosa heshima kwa wapinzani wako. Kisaikolojia tupo vizuri hasa baada ya kuwashinda Real Madrid wiki iliyopita kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini si ajabu ikatupa shida kwenye mechi hii.

“Villa wapo vizuri, wamejipanga na timu ipo imara. Si mchezo hawa kwa sababu wana golikipa mzoefu Pepe Reina lakini wana washambuliaji wenye kasi pale mbele Samatta na Grealish, wamejengeka vyema katika kiungo, wana wapiga vichwa wazuri na mabeki wa kati ni mahiri.

Samatta katika mechi yake ya kwanza na Aston Villa walishinda na kufanikiwa kutinga fainali ya Carabao Cup. Samatta aliyesajiliwa kwa pauni milioni 10 kutoka Genk wa Ubelgiji, alionesha soka safi na mechi kumalizika kwa ushindi dhidi ya Leicester ambao kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) wapo juu na wana nguvu sana.

Samatta alipongezwa na kocha wake, Dean Smith, aliyetangaza mapema kabla ya mechi kuwa atamchezesha baada ya kuridhishwa na jitihada zake kwenye mazoezi licha ya kuwa magumu kuliko ilivyo huko Genk. Samatta katika mechi ya leo anaweka tena rekodi ya kukanyaga Uwanja wa England, Wembley, ambako si wengi hufika kwa sababu huchezwa fainali za mashindano kama Kombe la FA, Kombe la Ligi na mechi za kimataifa.

Kocha wa Villa, Smith anasema haogopi kukabiliana na timu kubwa kama City ,timu kubwa na tajiri sana England hata kama ni mara yao ya kwanza kufika hapo tangu 2010.

“Ni kweli kwa kiasi kikubwa tunapewa nafasi ndogo ya kushinda mchezo huu kwa sababu City ni timu ya kiwango cha kimataifa lakini naweza kutaja timu mbili ambazo haziwezi kuwa zinatarajiwa kushinda zikikabiliana na City.

“Ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri na juzi kati wamewafunga Real Madrid, haijalishi ni wachezaji gani wanaanza kwenye kikosi chao cha kwanza. Kocha wao ni mzuri pia, lakini wakati mwingine napenda kutopewa nafasi ya kushinda kwa sababu tunaweza kupambana vyema bila kuwa na lile shinikizo la watu kutarajia kushinda,” alisema Smith.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi