loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mechi za kimataifa kutoahirishwa

RAIS wa Fifa, Gianni Infantino amesema maisha ni muhimu kuliko soka lakini michezo ya kimataifa ya kirafiki iliyotarajiwa kuchezwa mwezi ujao haitaahirishwa kutokana na tishio la virusi vya corona.

England na Wales zina mechi za kirafiki, wakati Scotland, Ireland ya Kaskazini na Jamhuri ya Ireland zinacheza kufuzu kwa Euro 2020. “Afya ya watu ni muhimu zaidi kuliko mchezo wowote,” alisema Infantino na kuongeza:

“Wachezaji wamewasiliana na vyama vyao kwa sababu ya hofu na wana wasiwasi juu ya michezo katika mazingira hatarishi.”

Infantino anasema ana matumaini kuwa mechi za kimataifa za mwezi ujao zitaendelea kama zilivyopangwa.

“Lazima tuangalie hali hiyo na tunatumaini itapungua badala ya kuongezeka. Kwa sasa inaonekana kama bado inaongezeka.

“Ikiwa michezo itastahili kuahirishwa au kuchezwa bila watazamaji hadi itakapomalizika, basi lazima tupitie hiyo.”

Umoja wa vyama vya wachezaji kimataifa (Fifpro) wenye vyama 65, unasema kumekuwa na mazungumzo kati ya wadau mbali mbali wa mpira wa miguu kuhusu kubadilisha tarehe za mechi za kimataifa.

Katika mchezo wa kufuzu wa Euro 2020, Machi 26 na Machi 31, Scotland itacheza Israel, Ireland ya Kaskazini itakabiliana na Bosnia na Herzegovina, wakati Jamhuri ya Ireland itakutana na Slovakia. England itaialika Italia kwenye Uwanja wa Wembley, Mchi 27, kabla ya Denmark kutembelea London siku nne baadaye. Wales wana mchezo wa kirafiki nyumbani dhidi ya Austria na Marekani. Mechi kadhaa za kufuzu Kombe la Dunia katika Shirikisho la Soka la Asia, pamoja na mchezo wa nyumbani wa Australia dhidi ya Kuwait na Hong Kong itakayosafiri kwenda Iran zimepangwa kuchezwa mwishoni mwa Machi. Mchezo wa kufuzu wa nyumbani wa China dhidi ya Maldives tayari umehamishiwa Thailand na utachezwa bila mashabiki. Mechi za Ligi ya Mabingwa ya Asia zinazohusika na klabu za China, Guangzhou Evergrande na Shanghai Shenhua pia zimeahirishwa. Mechi tano za Italia Serie A zitachezwa bila mashabiki mwishoni mwa wiki hii pamoja na mechi ya nyumbani ya Juventus dhidi ya Inter Milan. “Fifpro inajali usalama wa wachezaji ambao wanaweza kuwa wazi na ugonjwa na ni hatari kwa mpira wa miguu kuwa gari la kueneza magonjwa,” umesema umoja, ambao unafanya kazi kwa niaba ya wachezaji zaidi ya 65,000. “Tunaelewa usumbufu uliopo baada ya kuzuka kwa Covid-19, Usumbufu ni mkubwa kuliko mpira wa miguu na tunapongeza utayari wa waandaaji wa mashindano kuchukua hatua madhubuti katika kipindi hiki.” Tottenham na West Ham wamesema wanafuata ushauri wa serikali kucheza bila mashabiki kwa kipindi hiki cha tahadhari, kocha wa Newcastle Steve Bruce, alisema wamezuia wachezaji kusalimiana kwa kushikana mikono. “Tumezuia kwa ushauri wa daktari, kwa bahati nzuri, tunaye daktari mzuri hapa na atatujulisha juu ya nini tunapaswa kufanya,” alisema. Zaidi ya watu 80,000 wameambukizwa virusi hivyo, ambavyo vilitokea China lakini vimeenea nchi zaidi ya 50, na kusababisha vifo vya karibu watu 2,800. Wagonjwa wengine watatu wa virusi hivyo wamethibitishwa nchini Uingereza Ijumaa, na kufanya jumla ya watu kuwa 19 nchini humo kuwa na maambukizi hayo. La Liga imeahirisha mechi za Valencia, mikutano na mikusanyiko ya umma na kufunga sehemu ambazo zinaweka wachezaji hatarini, makocha na wafanyakazi wa klabu baada ya baada ya kubainika kuwapo kwa maabukizi ya Corona jijini humo. Michezo mingine iliyoahirishwa ni pamoja na rugby ya mataifa sita na China Gran Prix .

YANGA leo watakuwa ugenini kucheza dhidi ya wakata miwa wa ...

foto
Mwandishi: Zurich,Switzerland

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi