loader
Picha

Tanasha alianzisha kwa Diamond

MSANII Tanasha Donna, raia wa Kenya ambaye ni mpenzi wa msanii, Nassib Abdul ‘Diamond Platimuz’ amefuta picha za mpenzi wake katika ukurasa wake wa Instagram bila ufafanuzi wowote.

Tanasha ambaye pia ni mzazi mwenzake na Diamond walianza uhusiano wa kimapenzi mwaka juzi na wamezaa mtoto mmoja wa kiume.

Kwenye ukurasa wake huo, Tanasha aliandika ujumbe kuwashauri wanawake kuwa makini wanapoingia kwenye mahusiano ya kimapenzi, ujumbe ulioashiria mapenzi yake na Diamond kuwa na dosari.

“Wanawake kumbukeni mapenzi, ubinafsi, vitisho, uongo, kudharau hisia, wakati mwingine inachukua muda mrefu kujifunza, kushughulika na wabinafsi ni kama ushetani “aliandika Tanasha.

Tanasha ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio NRG nchini Kenya alifika mbali baada ya kuacha kuwafuata kwenye mtandao wa Instagram mama yake Diamond, Sandra na dada yake, Esma.

Chanzo cha mgogoro huo inasemekana Tanasha amemwona Diamond mbinafsi baada ya wiki iliyopita kutoa wimbo wake unaoitwa Jeje bila kuacha kwanza kupisha wimbo wa Gere aliomshirikisha ambao ulitoka mwezi uliopita na kupokelewa vema na mashabiki.

MWIMBAJI wa muziki wa Taarab, Khadija Kopa amesema anatarajia kuwania ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

3 Comments

 • avatar
  Jafet
  03/03/2020

  0629296277

 • avatar
  jackobkulwa58@gmail.com
  04/03/2020

  H

 • avatar
  Omary muja
  04/03/2020

  Waachane kwani ndo tabia ya mastaa wa bongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi