loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ubingwa wampa nyodo Guardiola

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema utawala wa timu hiyo kwenye michuano mbalimbali England unaendelea baada ya kushinda Kombe la ligi kwa mara ya tatu mfululizo.

Mabao ya Sergio Aguero na Rodri yaliipa ushindi City kabla ya Mtanzania Mbwana Samatta kuifungia timu yake Aston Villa bao moja katika matokeo hayo ambayo City ilishinda kwa mabao 2-1.

Mbali na ubingwa mara tatu wa Kombe la Ligi, Guardiola ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu, Kombe la FA na mawili ya Ngao ya Jamii akiwa na City. “Tangu tuanze kushinda, michuano tisa ya ndani ambayo tumecheza, tumeshinda mataji manane,” aliiambia BBC Radio 5 Live.

“Historia hii ni ya kushangaza. Kabla ya makombe ya ndani hakuna klabu yoyote katika historia yake, licha ya kutoshinda taji la Ulaya lakini imeshinda mataji kama tuliyoshinda sisi.”

“Si Liverpool kwenye miaka ya 80, Manchester United ikiwa na Sir Alex Ferguson au Jose Mourinho na Chelsea, au Arsene Wenger na Arsenal.” “Klabu hizi zilikuwa za kushangaza lakini hazikushinda mataji tisa, manane ya nyumbani.”

Liverpool ilishinda mataji sita ya ligi, Kombe la FA mawili na makombe manne yaliyofuata ya ligi miaka ya 1980, wakati United ilikusanya mataji 13 ya Ligi Kuu pamoja na matatu mfululizo mara mbili chini ya Ferguson, huku Wenger akiiongoza Arsenal kwenye kutwaa taji la ligi bila kufungwa.

Guardiola, ambaye alijiunga na Manchester City mwaka 2016, aliongoza timu yake kutwaa taji la Ligi Kuu, kombe la FA na kombe la ligi msimu uliopita, akiwa ameshinda pia ngao ya jamii kabla ya kuanza msimu mpya.

Mhispania huyo alisema hawezi kushindania taji la Ligi Kuu msimu huu kwa sababu Liverpool imewaacha mbali kwa pointi lakini anaamini wachezaji wake wataendelea kushinda mataji na kuifanya City kuwa klabu kubwa.

“Kabla hatujaenda Madrid, na Ulaya na kushinda kama tulivyofanya,” alisema Guardiola akizungumzia kikosi chake kilivyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Madrid kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya 16 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

“Hiyo haimaanishi tulistahili, lakini hii ni hatua ya kwanza. Kuamini tunaweza kwenda huko kucheza na kushinda. Hii ni muhimu zaidi kuliko kufika mwisho wa msimu tumeshinda taji moja au mawili.”

City ilitawala mchezo lakini Aston Villa ingepeleka mchezo huo kwenye muda wa nyongeza kama kichwa cha Bjorn Engels kisingeokolewa na Claudio Bravo. Kocha wa Villa, Dean Smith alisema anajivunia juhudi za wachezaji wake dhidi ya timu bora za juu duniani.

“Tulijua tungelazimika kuwa na subira bila mpira,” alisema Smith ambaye alikiri alidhani kichwa cha Engels kitaingia. Vijana wameonesha moyo mkubwa na ubora pia.” Ushindi wa West Ham na Watford kwenye mechi za ligi mwishoni mwa wiki iliyopita uliifanya Villa kuwa kwenye ukanda wa kushuka daraja licha ya kuwa na mchezo mkononi. Lakini Smith anajiamini ubora walionesha Wembley utawaondoa kwenye ukanda wa kushuka daraja.

“Huwezi kuangalia matokeo ya jana (juzi) kwa sababu hatukucheza, tuna mchezo mmoja mkononi na tukifanya mazoezi kuanzia leo tutaingia kwenye ligi tukiwa sawa.”

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amewataka mashabiki wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi