loader
Dstv Habarileo  Mobile
‘Urusi haina mpango wa kupigana na nchi yoyote’

‘Urusi haina mpango wa kupigana na nchi yoyote’

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin (pichani) amesema nchi yake haitapigana na nchi yoyote na inaweka misingi ili nchi zingine nazo zisiwe na msukumo wa kusababisha migogoro ya silaha na Urusi.

Putina alisema Urusi inashika nafasi ya saba ulimwenguni kwa matumizi ya kiulinzi ikitanguliwa na Marekani, China, Saudi Arabia, Uingereza, Ufaransa na Japan. Hata hivyo, alisema kuwa matumizi yao kijeshi kwa mwaka yanashuka ikilinganishwa na nchi zingine ambazo matumizi yake yanapanda.

“Hatutapigana na mtu yeyote. Tunakwenda kuweka mazingira ambayo hakuna mtu atakayetaka kupigana na sisi,”alisema Putin.

Alisema Urusi haiko tena nyuma tena kuhusu uwezo wake wa kiulinzi. Alisema kwa mara ya kwanza Urusi imeunda mifumo ya kushambulia ambayo ulimwengu haujawahi kushuhudia na sasa wanakimbia wakijaribu kuwafikia na kuongeza kuwa hilo ni jambo la kipekee na halijawahi kutoke hapo kabla.

Putin alisema hayo akirejea uundwaji wa mifumo mipya ya mashambulizi ya kasi ikiwemo ya kuvuka bara moja hadi jingine.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/33e041fbb4909d2c6b1d41409a7b50c8.jpg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi