loader
Dstv Habarileo  Mobile
Biden aibuka kidedea kuchuana na Trump

Biden aibuka kidedea kuchuana na Trump

MAKAMU wa Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden, aliyeshinda kwa kishindo kinyang’angi’ro cha kuwania nafasi ya urais kwa chama cha Democrat, amempiku mpinzani wake, Vermont Sandres.

Kwa matokeo hayo, sasa Biden atakutana kwenye kinyang’anyiro cha urais na Rais Donald Trump mapema Novemba mwaka huu wakati wananchi wa nchi hiyo watakapoamua ni nani awe Rais wa taifa hilo katika kipindi kingine.

Biden ambaye awali aliibuka mshindi kwenye Jimbo la South Carolina, pia ameibuka mshindi katika majimbo tisa kati ya 14 ya nchi hiyo yaliyopiga kura kumchagua nani apeperushe bendera ya Democrat kwenye uchaguzi ujao dhidi ya Republican. Biden, alikuwa hajawahi kushinda kwenye jimbo lolote katika uchaguzi huo wa awali wa urais mara tatu hadi mafanikio hayo ya Jumamosi.

Lakini utafiti wa maoni kabla ya uchaguzi unaonesha kwamba Sanders, mwenye mlengo wa kushoto wa kisoshalisti aliyejitangaza kugombea kupitia chama cha Democratic, alikuwa akiongoza kwa kura nyingi kwenye jimbo la Califonia lakini mwisho wa siku, Biden akambwaga chini. Majimbo ambayo Biden ameshinda ni Texas, North Carolina, Massachusetts, Minnesota, Oklahoma, Arkansas, Alabama, Tennessee na Virginia.

Hata hivyo Sanders alishinda jimbo la Califonia na majimbo mengine matatu. Kwa maana hiyo macho yote sasa yanaelekea Novemba ambapo nchi hiyo itafanya uchaguzi wa kumpata Rais kwa Awamu nyingine.

Awali, Meya wa zamani wa South Bend, Indiana, Pete Buttigieg alijiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais wa Marekani mwaka 2020. Timu ya Kampeni ya Meya huyo, ilitanganza juzi kwamba mgombea wao ameamua kujiondoa baada ya kumaliza katika nafasi ya nne ambapo hakupata wajumbe wa kumuunga mkono.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5c62bf8a56661879c26981689e4cf53f.jpg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: South Carolina, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi