loader
`City bado inaweza kufanya vizuri’

`City bado inaweza kufanya vizuri’

MANCHESTER City bado inaweza kuwa na "msimu wenye mafanikio " licha ya kuweka rehani taji lake la Ligi Kuu ya England, anasema mshambuliaji Raheem Sterling.

Kikosi cha Pep Guardiola, ambao ni mabingwa misimu miwili iliyopita, wako pointi 22 nyuma ya vinara Liverpool wakati akiingia uwanjani leo kucheza na majirani zao na wapinzani wao wakubwa Manchester United.

Man City ambao tayari wametwaa taji la Carabao na wamebaki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na Kombe la FA. Sterling aliuambia mtandao wa Football Focus kuwa kampeni za ligi "zinakatisha tamaa". Alisema: "Ligi Kuu ni tamu na chungu, Liverpool kwa sasa wako katika nafasi nzuri kuliko timu yeyote ile.

"Siwezi kusema kuwa tumekata tamaa, hatuna muendelezo wa kutosha kwa muda mrefu. Bado hatujaliachia taji.”

Man City msimu uliopita ilitwaa mataji matatu na Jumapili iliyopita iliifunga Aston Villa kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa taji la tatu mfululizo la Ligi. Wako mbele ya mabingwa mara 13 wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kuifunga Real Madrid kwa mabao 2-1 nyumbani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora na sasa watakabiliana na Newcastle katika mchezo wa robo fainali wa Kombe la FA.

Liverpool kwa sasa inahitaji kushinda mechi nne tu kati ya 10 ili iweze kutangazwa bingwa mpya wa Ligi Kuu ya England, taji ambalo walilitwaa kwa mara ya mwisho miaka 30 iliyopita. "Mara zote ni vizuri kutwaa taji, " alisema Sterling.

"Sasa biashara imemalizika na tuna mambo mengi ya kugombania. Kombe moja tumeshapoteza lakini tunajiamini tunaweza kufanya mambo makubwa msimu huu…”

"Ikiwa hautashinda mataji basi utamaliza msimu ukiwa umekata tamaa. Lengo letu ni kushinda kila taji la kila mashindano tunayoshiriki. "Tunaweza kumaliza katika nne bora na kushinda mataji mengine mawili. Bado unaweza kuwa msimu mzuri.”

MARA NNE

Hii ni mara ya nne kwa Manchester United kukutana na Manchester City msimu huu, wakati timu hizo zitakapokutana katika Uwanja wa Old Trafford. Kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kinaweza kushinda mara ya tatu endapo kitashinda mchezo huo ambao ni wa 182 tangu timu hizo zianze kukutana, lakini United ikishinda mechi zote kwenye Uwanja wa Etihad.

MWAMUZI WA MCHEZO

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu, utachezeshwa na mwamuzi Mike Dean. Mwamuzi huyo ana uzoefu mkubwa na tayari ameshachezeshamechi zaidi ya 500 tangu mwaka 2000, pamoja na mechi tano za debi ya Manchester. Dean atakuwa akisaidiwa na Darren Cann na Dan Robathan, huku mwamuzi wa mezani akitarajiwa kuwa Andre Marriner, ambaye atashughulikia VAR, akisaidiwa na Stephen Child.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/49a4b6496dadd9ec74ecd612e8ba3679.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi