loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kikwete akumbuka alipoanzia safara ya urais

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amefurahishwa na ujenzi wa ukumbi wa jengo la kitega uchumi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani na kukumbuka siku alipotangaza nia ya kuwania Urais.

Anasema alitangaza nia ya kuwania Urais kwenye Ofisi ya CCM Mkoa, kwenye mti wa mkungu uliopo mbele ya ofisi hiyo iliyopo wilayani Kibaha, na kuchaguliwa mara mbili kuongoza Tanzania.

Aliongoza Tanzania kutoka mwaka 2005 hadi 2005 Anasema mahali hapo panamkumbusha falsafa yake ya ‘Ari Mpya, Nguvu Mpya Kasi na Tanzania Yenye Neema Tele Inawezekana’, ambazo Aliyasema hayo wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa CCM uliopo eneo la Mkoani, Harambee hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Wauguzi mjini Kibaha.

“Nimekumbuka mbali ule mti wa mkungu, nina historia nao kwani hotuba yangu ya kwanza ya kuomba ridhaa ya kuwa Rais nilitangazia pale. Kwangu ni historia kubwa ambapo historia yangu iliandikwa pale kwani baada ya hapo ndipo nikaingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Urais,” alisema Kikwete.

“Niliitolea pale taarifa yangu…niliandaa usiku mwanangu Ridhiwani anaandika kwenye laptop (kompyuta mpakato). Sehemu ile nina uhusiano nayo katika safari yangu ya kisiasa, nauheshimu sana mkungu maalumu, kwangu safari ya mimi kuwa Rais ilianzia pale nilipoamua kugombea Urais. Wengine walikuwa wakitangazia Urais kwenye mahoteli, mimi niliamua kutangaza kwenye Ofisi ya CCM Mkoa,” amesema Kikwete.

Kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Kikwete aliwashinda wagombea wa vyama vingine vya upinzani ambao ni Paul Kyara (SAU), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Emmanuel Makaidi (NLD), Freeman Mbowe (CHADEMA), Augustine Mrema (TLP), Christopher Mtikila (DP), Dk Sengondo Mvungi (NCCR-Mageuzi), Anna Senkoro (PPT-Maendeleo) na Leonard Shayo (Demokrasia Makini).

Akizungumzia kuhusu ukumbi huo, alisema ni jambo jema na linapaswa kuungwa mkono na wanaCCM na wananchi kwa ujumla na kikubwa ni kuhakikisha ushirikiano unafanyika baina ya chama na wadau ili kufanikisha ujenzi huo.

“Uongozi mpya wa CCM Mkoa wa Pwani umeleta ari kubwa ya ujenzi wa ukumbi huu. Wazo lilikuwa ni la muda mrefu miaka mingi iliyopita na sasa naona ujenzi unaelekea kukamilika,” amesema Kikwete.

Amekishauri chama kuhakikisha kinakuwa na hati miliki ya viwanja vyake ili kuepuka watu kuyavamia maeneo yanayomilikiwa na CCM ili kuwa chini ya himaya kisheria. Aliahidi saruji mifuko 200 kuunga mkono ujenzi huo.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi