loader
Picha

Corona yatikisa soko Kenya

TANGAZO lililotolewa na Wizara ya Afya ya Kenya la kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza wa corona, limesababisha soko la bidhaa za kilimo na wanyama, kuyumba kwa kiasi kikubwa.

Hadi jana mchana kulikuwa na watu watatu nchini humo waliothibitika kuwa na virusi vya corona

Hii ni kutokana na masharti yaliyoandamana na tangazo hilo, yakiwemo kupigwa marufuku kwa mikusanyiko mbalimbali, ikiwemo masoko mbalimbali ya nchi hiyo.

Tangazo hilo lilitaja maeneo ambayo yapo katika hatari kubwa ya kusambaa kwa virusi hivyo vya COVID- 19 ni maduka makubwa, masoko, ofisi za umma na binafsi, benki, makanisa, misikiti, shule na vyuo vikuu.

Masoko makubwa katika miji ya Nairobi, Mombasa, Kisumu na Nakuru, yameonekana kukosa watu, hali iliyosababisha bidhaa nyingi, kukosa wateja na kuleta hatari ya bidhaa hizo kuharibika.

Bidhaa hizo ni mboga za majani, matunda, nyama na vinjwaji baridi. Baadhi ya masoko yaliyokuwa yakitegemea kampuni kubwa, kuagiza bidhaa kutoka China, yanapata tabu kutokana na kukosa bidhaa kwa muda mrefu sasa.

Wizara ya Afya ya Kenya inawasisitiza wananchi kuendelea kuuza na kununua bidhaa za nyumbani bila kuwa na wasiwasi wowote.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: MOMBASA, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi