loader
Picha

Waumini wafundishwa kujikinga corona

MAKANISA nchini Kenya, yameanza kuchukua tahadhari kwa kuwafundisha waumini wao namna bora ya kujikinga na virusi hatari vya corona.

Makanisa yameshuhudiwa mwishoni mwa wiki, yakiweka utaratibu kwa kila muumini kunawa mikono kwa sabuni maalumu, inayotajwa kuwa na dawa yenye kuangamiza vimelea vya ugonjwa wa corona.

Mfano katika jiji la Nairobi, Kanisa la Karura lenye uwezo wa kuchukua waumini zaidi ya 2,000, lilikuwa likitoa huduma ya kunawa mikono kwa sabuni maalumu kwa waumini wake.

Hatua hiyo ni kielelezo kizuri cha nyumba za ibada zinazowakinga waumini wake na ugonjwa huo hatari.

Mchungaji wa kanisa hilo, George Shirambo aliwaambia waandishi wa habari kuwa ni jukumu la kanisa kuhakikisha kuwa waumini wanakuwa salama, kuanzia wanapoingia kanisani hadi wanapoenda nyumbani wakiwa salama.

Hatua hiyo imeanza kuchukuliwa na makanisa yote nchini Kenya katika miji mbalimbali, ikiwemo mji wa Mombasa.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi