loader
Picha

Fomu za wagombea 4 urais zakataliwa

FOMU za wagombea wanne kati ya 10 katika nafasi ya urais, zimekataliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kutokidhi mahitaji yanayotakiwa. Wagombea hao waliokataliwa, wamesema watakata rufaa katika Mahakama ya Katiba.

Wagombea ambao fomu zao za kugombea zimekataliwa ni Jacques Bigirimana ambaye ni mgombea urais wa chama cha FNL na mgombea wa Chama cha CDP, Anicet Niyonkuru.

Wengine ni mgombea wa chama FPN-Imboneza, Valentin Kavakure na Rais wa zamani, Domitien Ndayizeye wa chama cha Kira cha Umoja wa vyama. Mwenyekiti wa NECI, Claver Kazihise, alisema tume haikukubali fomu zao kwa sababu wagombea hao hawakukidhi mahitaji stahili ya katiba na sheria za uchaguzi.

Walipewa siku mbili kukata rufaa. Ndayizeye alisema anashangazwa na maamuzi hayo. Anicet Niyonkuru kutoka chama cha CDP alitangaza kuwa watakata rufaa katika Mahakama ya Katiba.

Miongoni mwa wagombea sita waliokubaliwa fomu zao na CENI, kwa ajili ya kugombea uchaguzi mkuu Mei 20 ni Evariste Ndayishimiye (kushoto) wa chama tawala cha CNDD-FDD, na Agathon Rwasa (kulia) wa chama kikuu cha upinzani cha CNL.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi