loader
FKF yamuomba Rais Uhuru awalipie deni

FKF yamuomba Rais Uhuru awalipie deni

SHIRIKISHO la Soka Kenya (FKF) sasa limegeukia kwa Rais Uhuru Kenyatta kuhusu malipo ya Sh milioni 109 wanayodaiwa na kocha wa zamani wa Harambee Stars, Adel Amrouche baada ya kumtimua bila kufuata taratibu.

Rais wa FKF, Nick Mwendwa mwishoni mwa wiki alimuomba Rais wa Kenya kuwalipia deni hilo ili kuinusuru Kenya isifungiwe na Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa).

“Mtu mmoja alifanya makosa na sitaki kufikia hatua ya kumtaja. Napenda kumuomba Rais kusaidia kulimaliza hili deni la Sh milioni 109,” alisema Mwendwa wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Kenya kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo jijini hapa.

Kwa FKF kushindwa kumlipa Amrouche kabla ya siku ya mwisho waliyopewa ya Machi 11 ambayo iliwekwa na Fifa, Kenya inaweza kukumbana na rungu la kufungiwa kushiriki mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022.

Wiki iliyopita, Waziri wa Michezo, Amina Mohamed alisema kuwa ni upuuzi mkubwa kwa FKF kufikiria kuwa ni jukumu la serikali kumlipa kocha. FKF imesema kuwa haina fedha za kumlipa kocha huyo Mualgeria.

“Sijui kwanini wanakuwa na mawazo potofu kuwa serikali ndio yenye jukumu la kumlipa kocha, hilo ni jukumu la shirikisho kumlipa kocha huyo,” alisema Amina.

“Serikali haina la kufanya kuhusu hilo. Kwanini FKF wasikubaliane na Fifa kuhusu mpango wa kumlipa kocha huyo,” alisema katika mahojiano hayo yaliyofanyika mapema.

Licha ya msimamo mkali wa Amina, Mwendwa alisema kuwa bado anazungumza na Wizara ya Michezo kuhusu suala hilo. Aliwaambia waandishi wa habari kuwa baada ya serikali kutochukua hatua yoyote hadi leo kwa sababu Sh milioni 109 ni kiasi kikubwa cha fedha, “Ni jambo muhimu kulipa deni hilo…”

Amrouche alitimuliwa mwaka 2014 baada ya kufungua kesi Fifa akitaka alipwe kiasi cha Sh milioni 60. Hata hivyo, FKF ilipokata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi ya Mambo ya Michezo (Cas), adhabu iliongezwa na kutakiwa kulipa kiasi cha Sh milioni 109.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5d0b7921bcf73463c13a0c8673660f2c.jpg

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi