loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mambo muhimu kuhusu corona

VIRUSI vya corona vilivyogundulika hivi karibuni, vinasababisha ugonjwa unaofahamika COVID-19. Ni jamii ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanyama na binadamu. Vinasababisha maambukizi kwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji.

Dalili kuu za ugonjwa huu ni homa kali, uchovu na kikohozi kikavu na zinatokea taratibu. Dalili inayotia hofu zaidi ni kukosa pumzi ingawa taarifa za kitaalamu zinasema mtu mmoja kati ya watu sita walioambukizwa ndiyo hufikia dalili hiyo. Shirika la Afya Duniani (WHO) inasema wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu kama vile shinikizo la damu, kisukari, matatizo ya figo ndiyo walio katika hatari kubwa kuathirika wanapopatwa na virusi vya corona.

Virusi vinaweza kusambaa kupitia maji maji kutoka kwenye pua au mdomo wa aliyeathirika. Kugusa mafua, mate na makohozi ya mwenye virusi na kisha kujigusa mdomo, macho na pua kunaweza kusababisha kupata virusi vya corona. Ili kujikinga virusi vya corona, inapaswa kunawa kila wakati mikono kwa maji ya vuguvugu, sabuni au dawa za kuua vijijidudu. Kaa umbali wa angalau hatua mbili kutoka mtu anayepiga chafya au kukohoa.

Epuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi. Zingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya. Iwapo una mafua makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kupata msaada wa kitaalamu. Epuka kuwa sehemu yenye msongamano kama vyombo vya usafiri, maduka na maeneo yenye mgandamizo wa hewa. Tumia kifunika mdomo na pua na ukivae kwenye mikusanyiko.

Hadi sasa hakuna tiba au chanjo dhidi ya virusi vya corona na vinampata mtu yeyote bila kujali rangi. Kwa mujibu wa takwimu zilizoripotiwa na BBC jana ikinukuu chuo kikuu cha Johns Hopkins, jumla ya wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo duniani ni 169,432 na vifo 6,513. Nchi zenye wagonjwa na vifo vingi ni China, Italia, Iran, Korea Kusini, Hispania, Ujerumani, Ufaransa, Marekani, Uswisi, Uingereza, Norway, Uholanzi, Sweden, Ubelgiji, Denmark, Austria na Japan.

Hadi jana, nchi 25 za Afrika ziliripotiwa kuwa na maambukizi ya corona. Miongoni mwake ni Misri, Algeria, Tunisia, Sudan, Ethiopia, Kenya, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda, Algeria, Eswatin, Afrika Kusini, Liberia, Eritrea, Cameroon, Ghana, Tunisia, Senegal, Algeria na Tanzania.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    said
    18/03/2020

    jamani tutumieni update za corona

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi