loader
Picha

Hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya wagonjwa wapya 2 kungunduliwa na Corona

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa leo ametangaza ongezeko la wagonjwa wawili wa virusi vya Corona nchini, mmoja akiwa ni raia wa Ujerumani (24) na wa pili ni Mmarekani (61).

Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema raia huyo wa Ujerumani alihisiwa kuwa na maambukizi akiwa Zanzibar na Mmarekani alibainika kuwa na virusi hivyo akiwa jijini Dar es Salaam.

Pia ametangaza kusitishwa masomo vya vyuo vya elimu ya kati na vyuo vikuu nchini ili kuondoa misongamano vyuoni.

“Leo tunaendelea kuongeza vyuo vya elimu ya kati na vyuo vikuu nchini…navyo pia tunasitisha kuendelea na masomo,” – Waziri Mkuu, Kassim.

Majaliwa Kabla ya tangazo hilo la kusitisha masomo ngazi ya elimu juu na vyuo vya kati, Waziri Mkuu alitangaza jana kufungwa shule zote za awali, msingi na sekondari nchi nzima.

“Kati ya maeneo ambayo tulikuwa tumesitisha kuendelea na shughuli, ilikuwa ni kuzifunga shule zote za awali, msingi na sekondari,” - Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Hata hivyo, Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania kuwa makini na kutokuwa na taharuki na kuwataka kuendelea na shughuli zao za kila siku huku serikali ikipambana kuhakikisha ugonjwa huo hausambai nchini.

Mtu wa kwanza kukutwa na virusi vya Corona nchini Tanzania, ni mwanamke Mtanzania wa miaka 46 aliyetokea nchini Ubelgiji na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Jumapili iliyopita, Machi 01, Mwaka huu.

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk ...

foto
Mwandishi: Isdory Kitunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi