loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Viwanda 50 Pwani kuunganishwa umeme wa gesi

SERIKALI imesema iko kwenye mpango wa kuviunganishia umeme wa gesi viwanda 50 kwenye mikoa mitatu inayopitiwa na miundombinu ya gesi kupunguza gharama. Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ambaye alimwakilisha Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani wakati Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea kiwanda cha Lodhia Group kilichopo Mkuranga mkoani pwani. Alisema mpango kazi wa TPBC wa matumizi ya gesi asilia ni kuhakikisha viwanda vipya 50 vimepitiwa na bomba la gesi ikiwemo Dar e Salaam, Pwani na Mtwara.

“Mkoa wa Pwani ulianza Mkuranga mwaka 2018 ambapo kiliunganishwa kiwanda cha Goodwill ambapo kiwanda cha Knauf kazi inaendelea kwani malengo ni kuhakikisha kunakua na watumiaji wengi kwani gesi ipo nyingi na ya kutosha,”alisema Mgalu.

Alisema serikali kupitia taasisi zake inawezesha sekta ya viwanda kwani inaongeza ajira na mapato kwa serikali na sekta ya viwanda ikiimari- ka hata uchumi wa nchi utakua na itaaendana na mkakati wa serikali ya awamu ya tano kuwa nchi ya viwanda.

“Tumeona moja ya changamoto ya viwanda ni umeme lakini hali hiyo itakwisha kwani mradi wa uzalishaji umeme wa Nyerere Rufiji itakuwa mkombozi, gharama za umeme zikishuka za uzalishaji zitapungua na bei za bidhaa zitashuka,” alisema Mgalu.

Aidha alisema watahakikisha wanasimamia vyema mradi wa Nyerere ili gharama za umeme zishuke na mwingine kuuzwa nje ikiwemo Kenya kutokea Singida- Namanga. Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Vedastus Mathayo alisema wamefurahi kwani zamani walinunua vitu Uturuki kupata ubora lakini sasa vifaa vinapatikana hapa. Alisema changamoto ni kuwa bei ya umeme iko juu hivyo umeme wa mradi wa Julius Nyerere utapunguza gharama ili ziwe chini bidhaa zizalishwe hapa na kuuzwa nje.

“Tumewaambia walete gharama maeneo mengine wanakouza bei ndogo kama Afrika Kusini. Pia tumeona kuna kiasi kidogo cha vyuma chakavu hivyo inabidi anunue kutoka nje na kibali kinachukua zaidi ya miezi mitatu na oda mwaka mzigo kufika,”alisema.

Mmiliki wa kiwanda hicho, Harun Lodhia alisema zamani walikuwa wanatumia oili chafu iliyochafua mazingira lakini sasa na wana mradi mkubwa wa kupata mashine ya kubadili umeme wa gesi kuwa wa kawaida unaogharimu Sh bilioni 10 mwaka moja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Mkuranga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi