loader
Picha

Nusu ya wagonjwa wa corona wapona, waruhusiwa

NAIBU Mkurugenzi wa Hospitali ya Leishenshan ya Wuhan, Yuan Yufeng amesema karibu nusu ya wagonjwa wa homa ya virusi vya corona (COVID-19), waliopewa matibabu katika hospitali hiyo wamepona na kuruhusiwa.

Yuan alitoa kauli hiyo mjini humo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya ugonjwa huo. Alisema wanashukuru jitihada zilizofanywa kuudhibiti, zimezaa matunda, kwani zaidi ya nusu ya wagonjwa waliokuwa wakitibiwa, wamepona na wameruhusiwa kurudi kwao.

Yuan alisema hadi kufikia Machi 16 mwaka huu Hospitali ya Leishenshan, ilikuwa imepokea wagonjwa 1,961 wa COVID-19 na wagonjwa 970 kati yao tayari wameruhusiwa.

“Tulipokea wagonjwa wa COVID-19 wapatao 1,961 na hadi Machi 16,mwaka huu wagonjwa 970 kati ya hao walitibiwa na kupona na wameruhusiwa,” alisema Yuan.

Alisema kuwa hospitali hiyo ina wafanyakazi wa matibabu 3,202 wa timu 16 za matibabu kutoka mikoa tisa na wahudumu 660. Kwamba mapambano dhidi ya ugonjwa huo, bado yanatiliwa mkazo na msisitizo

KIWANGO cha mimba za utotoni kimeripotiwa kupungua kwa kasi katika ...

foto
Mwandishi: WUHAN, China

2 Comments

 • avatar
  JUMANNE
  19/03/2020

  Comment Hogera selekali ya tanzania kwa hatua za haraka kufunga tasisi mbalimbali wenzetu huko china wagonjwa 970 wamepona waziri ummy fatilia hiyo dawa waliyo tumia kuponyesha mama tutaasilika kiuchumi

 • avatar
  Karoli Thomas
  19/03/2020

  Ugojwa wakorona simzu kwa binadamu kinachotakiwa ni kuuthibit halaka iwezekanavyo sivyo tutapotea wote

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi