loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lukaku: Ole alitaka nibaki Man United

ROMELU Lukaku anasema kuwa “hakuwa na nguvu “ ya kubaki Manchester United licha ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kumtaka kubaki Old Trafford alipokuwa akitaka kuhamia Inter Milan.

Uhamisho wa Lukaku kwenda Ligi Kuu ya Italia, Serie A Agosti mwaka jana ulimaliza uwepo wake wa miaka miwili pale Old Trafford ambapo alishuhudia kiwango chake kikikosolewa, hasa msimu wake wa pili katika klabu hiyo. Kocha wa Man United, Solskjaer alisema Septemba mwaka jana kuwa ulikuwa ni uamuzi sahihi kumuachia Lukaku kuondoka, kwani hatua hiyo ingetoa nafasi kwa chipukizi Mason Greenwood.

Katika mahojiano ya YouTube na Ian Wright, Lukaku alisema: “Mwaka mmoja mbaya unaweza kutokea kwa kila mtu katika kazi yake. Na hili ndilo lilitokea kwangu. Unajua kilichotokea nyuma ya pazia. Kwangu hilo lilitokea.

“Ilikuwa hali ngumu ambako mimi mwenyewe ilibidi kufanya uamuzi wapi nitakapokwenda, hivyo nitajifunza vitu vingine tofauti kuhusu mchezo wangu na kazi na mtu ambaye ananihitaji.

“Ole alikuwa akitaka mimi nibaki, lakini nilimwambia inatosha, sina nguvu tena. Shukrani zote kwake kwa sababu ni mtu aliyenisiadia mimi kuondoka.”

Baada ya changamoto mwanzoni mwa msimu, kiwango chake kilipanda na kuifanya timu kuwa katika mbio za kuwania kumaliza katika nafasi nne za kwanza, wakati mashinda yaliyobaki ya Kombe la FA na Ligi ya Ulaya kabla ya kusimamishwa kutokana na kueneo kwa virusi vya corona.

“Wanakwenda katika muelekeo mzuri kwa sababu wameleta wachezaji sahihi,” alisema Lukaku.

“Ole anafanya kazi nzuri na matokeo yako upande wao. Hakuna kingine ninachowatakia zaidi ya mambo mazuri. “Ni klabu ambayo imenipatia msingi imara, ambao sijawahi kuuona maishani mwangu, hivyo, kwangu ni kuhusu kutoiheshimu Man United au klabu nyingine yoyote ambayo niliichezea nikiwa England nafikiri huo ni utoto,” Lukaku alifunga mabao 42 katika mechi 96 alizoichezea Man United, lakini amefunga mabao mengi tangu alipotua Inter, ambako amefunga mabao 23 katika mechi 35.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alibainisha kuwa ilikuwa “karibu” kutua kwa mahasimu wa Inter au wapinzani wa Serie A Juventus, lakini ni kocha wa Milan Antonio Conte aliyefanya jitihada kubwa kwa mchezaji huyo kufikia uamuzi huo. “Ilikuwa karibu. Kwa kweli ilikuwa karibu lakini akili yangu ilielekea Inter…na kocha,” alisema Lukaku. “Nilipokuwa mtoto, Inter ilikuwa ni timu yangu Italia. Nilikuwa nawaangalia Adriano na Ronaldo.

“Ni wazi Inter walipokuja, kocha wao Conte alikuwa akinitaka mimi Chelsea na alipokuwa Juve…” Mchezaji hiyo wa zamani wa Chelsea alibainisha kuwa ameshindwa kumuona mama yake, ambaye anaugua ugonjwa wa sukari, na hajamuona mtoto wake mdogo wa kiume. “Kwa kweli nimeyakosa maisha ya kawaida,”alisema Lukaku. “Kuwa na mama yangu, kuwa na mtoto wangu wakiume, kuwa na kaka yangu.”

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi