loader
Picha

Mianzi fursa nzuri uchumi wa viwanda

MIANZI ni mimea inayopatikana katika katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na nchini Tanzania imekuwa ikipatikana karibu mikoa yote, isipokuwa mkoa wa Lindi ndio wenye mianzi mingi kuliko mingine.

Lakini pia mikoa ya Iringa na Njombe na jiji la Dar es Salaam, mianzi ya njano imekuwa ikilimwa, lakini mingi ikitumika kwa shughuli za kawaida ikiwemo kutengeneza mvinyo wa asili maarufu kama ulanzi Duniani bidhaa zitokanazo na mianzi, zinatajwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni saba, lakini kwa Afrika thamani ya mianzi ni asilimia 1.2 tu ya dola hizo bilioni saba.

Kutokana na takwimu hizo, kuna fursa kubwa ya kutumia mmea huo kupata masoko katika nchi mbalimbali wanazotumia mmea huo kwa wingi, kwa shughuli mbalimbali ikiwemo uzalishaji bidhaa.

Nchi za EAC pia zinaweza kutumia mianzi kutengeneza bidhaa kwa ajili ya kukuza viwanda vya ndani .

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuhifadhi Wanyamapori na Mazingira Tanzania (WCST), Dk Felician Kilahama anasema katika kukamata soko hilo Tanzania tayari ina hekta 100,000 na tayari zimepandwa mianzi.

Juhudi kubwa inafanyika kupanda zaidi zao hilo lenye soko kubwa katika nchi mbalimbali ikiwemo China.

Bidhaa zinazotengenezwa kutokana na mianzi duniani ni nyingi, ingawa nchi za Bara la Afrika ziko nyuma katika kutengeneza na kutumia bidhaa za mianzi.

Nchi za Bara la Asia ndizo zinazoongoza kwa matumizi ya bidhaa za mianzi.

Katika nchi hizo, hasa China, mianzi hutengeneza samani , nguo, vyakula mbalimbali kama chocolate, ‘bamboo shoots’, mvinyo, dawa, mkaa, vijiti vya kulia chakula, vijiti vya kuchoma nyama, vijiti vya meno, ujenzi, baiskeli za mianzi na vikombe vya mapambo .

Wanunuzi wakubwa wa bidhaa za mianzi ni nchi za Umoja wa Ulaya (EU) , Hong Kong, Japan na Marekani. Nchi hizo kwa pamoja hununua kwa jumla asilimia 80 ya bidhaa za mianzi duniani.

Asilimia iliyobaki ndiyo inayotumiwa na mataifa mengine. Kutokana na takwimu hizo, ni dhahiri kuwa umefika wakati kwa nchi zingine za EAC kufuata nyayo za Tanzania, kwa kuanzisha mashamba ya mianzi na kuanzisha viwanda vidogo, kati na vikubwa vya kuzalisha bidhaa kwa kutumia mianzi.

Uwepo wa viwanda hivyo, utapunguza uingizaji wa bidhaa hizo katika EAC na kuwezesha kuuza bidhaa hizo nje ya EAC, hivyo kuongeza uchumi wa wananchi na wa nchi husika.

JUZI Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kamati za maafa katika ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi