loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Singida kutumia mil 550/- kupambana na corona

MKOA wa Singida unatarajia kutumia zaidi ya Sh milioni 550, kupambana na virusi vya corona, vinavyosababisha homa ya mapafu ya Covid-19. Hayo yamesemwa na Katibu wa Kamati ya Afya ya Msingi (PHC), Dk Boaz Balla.

Alisema hayo wakati akiwasilisha mpango mkakati wa dharura wa mkoa kupambana na virusi vya ugonjwa huo kwenye kikao kilichojumuisha wadau mbalimbali. Dk Balla alisema ushiriki wa kila mdau katika suala hilo ni muhimu, kutokana na changamoto za ugonjwa wa corona kuwa mtambuka. Alisema fedha zilizopangwa, zitatumika kuzuia kuingia na kuenea kwa ugonjwa huo kwenye jamii, kujenga uwezo wa uratibu wa kukabiliana na janga hilo na kuhudumia kwa haraka washukiwa wote wa covid-19.

Zitatumika pia kuimarisha ukusanyaji, utunzaji na usafirishaji wa sampuli za ugonjwa huo, kuhakikisha usalama wa watoa huduma na wateja, upatikanaji wa dawa, mawasiliano, uratibu na ushirikishwaji jamii. Kwa sasa mkoa hauna fedha hizo, hivyo wadau wametakiwa kusaidia kwa hali na mali, kukabiliana na ugonjwa huo. Alisema vita huwa havipiganwi na mtu mmoja na kwamba umoja ni nguvu katika kupiga vita corona.

Alionya matumizi holela ya barakoa. Alisisitiza kuwa barakoa hazipaswi kuvaliwa na kila mtu au kila mahali, bali zivaliwe na mtu aliyekumbwa na ugonjwa huo, au mtu anayemhudumia mgonjwa au watakaofika eneo walikotengwa wagonjwa wa aina hiyo. Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Paskasi Muragili alisisitiza umuhimu wa wadau wa ndani na nje ya mkoa, kuchangia mfuko huo wa dharura ili kufanikisha lengo la mkoa, kutokuathirika na maambukizi ya virusi vya corona.

Alisema kuwa mkoa wa Singida, una utajiri mkubwa wa bidhaa mbalimbali, vikiwemo vitunguu, ambavyo hufuatwa na wafanyabiashara kutoka nje ya nchi. Hivyo, kuna haja ya kuweka udhibiti wa hali ya juu kwenye eneo la soko hilo na maeneo mengine hatarishi, kama vile maegesho ya malori yaendayo maeneo mbalimbali na nje ya nchi.

Alisema kuna mwingiliano mkubwa wa kibiashara na kijamii kati ya Singida na mikoa mingine na nchi jirani, hivyo wanatakiwa kuchukua tahadhari. Alitaka wamiliki wa nyumba za kulala wageni, watoe taarifa sahihi za wageni wao, hasa wanaotoka nje ya nchi.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Singida

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi