loader
TB, ukoma kutokomezwa mwaka 2030

TB, ukoma kutokomezwa mwaka 2030

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga mwaka 2030 kuhakikisha ugonjwa wakifua kikuu na ukoma unatokomezwa ikiwa ni maelekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mkuu wa Kitengo Shirikishi cha ugonjwa wa kifua kikuu Zanzibar, Farhat Juma alisema hayo alipozungumza maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa TB mkoa wa Kusini Unguja. Alisema TB bado tishio kwa afya za wananchi wengi kutokana na mazingira wanavyoishi katika mfumo wa msongamano mkubwa.

‘’Wizara ya Afya ipo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa TB kuona kwamba unapigwa vita na kutokomezwa moja kwa moja,’’ alisema. Mratibu wa Kitengo cha TB na ukoma Zanzibar, Khamis Abubakar alisema mwaka 2019 watu 996 wameugua na vifo 39.

Alisema kitengo kinaendelea na mapambano dhidi ya TB ingawa mwamko wa wananchi katika kutokomeza ugonjwa huo bado mdogo. Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud aliwataka wananchi wa mkoa huo na wilaya zake kuchunguza afya zao mara kwa mara kujua kama wapo salama au la.

Alisema TB ni hatari ndiyo maana WHO imeamua kuchukua mikakati kuitokomeza.

‘’Njia za kukabiliana na TB ni kuchunguza afya za wananchi katika vituo vya afya,’’ alisema.

Takwimu za WHO zinaonesha TB ni kati ya maradhi 10 hatari yanayosababisha vifo. Aidha takwimu zinaonesha mwaka 2018 watu milioni 10 waliugua ugonjwa wa TB duniani huku watu milioni 1.5 wakipoteza maisha.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5cbbd27c4a2fda444ec9737871093250.jpg

Vituo vya afya vyafikia 8461Idadi ya Vituo vya ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi