loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magari Dar yapuliziwa dawa kuzuia corona

Upuliziaji dawa ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mapafu, unaosababishwa na virusi vya corona (Covid 19. ), ulianza jana katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam.

Lengo la upuliziaji huo ni kutekeleza agizo la serikali la kuhakikisha ugonjwa huo, hauenei zaidi katika jiji hilo kubwa nchini.

Akihojiwa na gazeti hili jana jioni, Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge, alisema walifanya kazi hiyo katika baadhi ya maeneo, kama vile katika mabasi ya mwendokasi, mabasi ya kawaida, magari ya watu binafsi na barabarani.

Mathalani kwenye mabasi ya mwendokasi, walikuwa wakipulizia dawa kwenye milango, sakafuni, madirishani na kwenye vyuma.

Hali ilikuwa hivyo hivyo kwenye mabasi mengine na magari. Kunenge alisema zoezi hilo, limelenga kudhibiti magonjwa matatu ambayo ni dengue, malaria na corona.

Kwa Manispaa ya Ilala, ofisa mmoja wa manispaa hiyo, alisema jana walikuwa wanafanya maandalizi na leo wataanza zoezi hilo katika maeneo mbalimbali.

WATAALAMU wa Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

JKCI yachunguza 150 shinikizo la damu Temeke

dakika 26 zilizopita Mwandishi Maalumu, Ukerewe

WATAALAMU wa Taasisi ya ...

Chagueni CCM, chama chenye mipango - Majaliwa

masaa 9 yaliyopita Mwandishi Wetu

MJUMBE ...

Mgombea CCM aomba kuchaguliwa tena

masaa 9 yaliyopita Alexander Sanga, Mwanza