loader
Picha

'Vyombo visivyokaguliwa visiende baharini'

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) mkoani Tanga, limetoa wito kwa vyombo vya usafi ri vinavyofanya kazi zake majini, ambavyo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora, kutokwenda majini kufanya shughuli zake.

Agizo hilo lilitolewa jana na Ofisa Mfawidhi wa shirika hilo mkoani Tanga, Christopher Shalua wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Shalua alisema wanatoa wito kwa vyombo vya majini kwa kipindi hiki cha masika, vyombo ambavyo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora haviruhisiwi kwenda majini.

Alisema pia kwa kipindi hicho, vyombo vyote vilivyopata vyeti vya ubora ni vizuri kuchukua tahadhari, kuhakikisha vifaa vyote vya umuhimu ikiwemo pampu za kutolea maji yaliyoingia kwenye chombo zinafanya kazi na zipo.

Aidha, alisema kwa vyombo ambavyo havitakuwa na vifaa vitakavyostahili kuruhusu kwenda majini, wanavitaka visiende kufanya shughuli zozote majini kwa kuchukua tahadhari.

“Tunatoa rai kwa vyombo kuzingatia maelelezo hayo kwa sababu kipindi cha masika kinaambatana na hali mbaya ya hewa mawimbi makubwa pamoja na mvua ambazo zinasababisha maji kuingia kwenye chombo na kusababisha uzito,” alisema.

Alisema hivyo kama uwezo wa kutoa maji kwenye chombo utakuwa ni mdogo, itakuwa rahisi kuzama. Alitoa wito kwa vyombo vyote hasa kwa uvuvi, maelekezo hayo yazingatiwe.

KIWANGO cha mimba za utotoni kimeripotiwa kupungua kwa kasi katika ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Tanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi