loader
Picha

Mgawanyo madaktari wapya 1,000 huu hapa

KATIKA kutekeleza agizo la Rais John Magufuli ya kuajiri madaktari, serikali imetangaza nafasi za 1,000 za ajira mpya za kada ya madaktari Daraja la II wakiwemo 610 watakaofanya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya tangazo la ajira iliyosainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dk Zainabu Chaula, ajira hizo zimetolewa ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Magufuli baada ya kutolea kibali cha ajira na kuwa mwisho wa kupokea maombi hayo ni Aprili 10, mwaka huu saa 9:30.

Rais Magufuli alipokutana madaktari nchini hivi karibuni, alitoa kibali cha kuajiri madaktari wapya 1,000 ili kutatua changamoto ya uhaba wa wataalamu hao wa afya nchini.

“Ninafahamu kuna madaktari karibia 2,700 hawajaajiriwa, nitalifanyia kazi. Nafikiri tunaweza tukaanza polepole hata tukachukua 1,000, sieti Waziri wa Utumishi (George Mkuchika), hatuwezi kuajiri hata 1,000? “Hela si zipo kidogo? Basi tuajiri 1,000 madaktari, tuanze na 1,000 mambo yakiwa mazuri tunaajiri wengine kwa sababu tunahitaji madaktari mpaka vijijini,” alisema Rais Magufuli wakati huo.

Dk Chaula aliutaja mchanganuo wa ajira hizo 1,000 kuwa ni madaktari 610 wa hospitali za zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amesema madaktari 306 wataajiriwa katika hospitali za Rufaa za Mikoa ambazo zinasimamiwa na Wizara ya Afya, madaktari 40 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam na madaktari 20 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Aliongeza kuwa katika ajira hizo, pia zitakuwepo nafasi 10 kwa ajili ya Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), madaktari saba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na madaktari saba kwa ajili ya Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), zote jijini Dar es Salaam.

Aidha, Dk Chaula alitaja sifa za waombaji kuwa ni awe raia wa Tanzania, awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45, na awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea.

“Pia awe hajawahi kuajiriwa serikalini na kupata cheki namba na endapo mwombaji atakuwa alishaajiriwa serikalini na kupata cheki namba atatakiwa kuzingatia utaratibu wa uhamisho au kurejea katika utumishi wa umma baada ya kuacha kazi kama alivyobainishwa kwenye Waraka namba CCB. 228/271/01 wa Agosti 7, mwaka 2012,” alieleza Katibu Mkuu Afya.

Alisema waombaji waliochaguliwa watapangiwa kazi kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa madaktari.

“Hivyo madaktari watatakiwa kuchagua maeneo matatu ambayo angependa kupangiwa endapo utafanikiwa kupata nafasi hiyo na pia nakala za vyeti zithibitishwe na mahakama au wakili"amesema.

“Waombaji ambao wanajitolea katika mikoa mbalimbali waambatanishe barua inayomtambulisha kutoka kwa Mganga Mkuu au mfawidhi wa mamlaka husika,” alieleza.

NAIBU Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi