loader
Picha

Mwingine akutwa na corona Zanzibar

WIZARA ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imethibitisha kuwepo kwa mgonjwa mwingine wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19) na kufanya idadi kufikia wagonjwa wawili.

Mgonjwa aliyetambuliwa ni mwanamke raia wa Ujerumani ambaye mumewe ni raia wa Ghana.

Mume wa mwanamke huyo amelazwa zaidi ya wiki mbili katika kituo cha kupokea wagonjwa wa Corona, Kidimni Wilaya ya Kati Unguja.

Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohamed alithibitisha taarifa wakati akizungumza na waandishi wa habari, akisema mgonjwa aliyelazwa alichukukuliwa sampuli pamoja na mumewe, lakini hakuonesha dalili za Corona.

“Mgonjwa aliyelazwa jana alichukuliwa sampuli yeye na mumewe lakini yeye hakuonesha dalili za ugonjwa huo... mumewe amelazwa katika kituo cha Kidimni kwa zaidi ya wiki mbili sasa na hali yake ni nzuri,” alisema Hamad Rashid.

Aidha, alisema watu 134 wanaendelea kuchunguzwa pamoja na kufuatiliwa nyendo zao kuhusu ugonjwa wa Corona ambao wengi ni wale waliorudi nchini ikiwemo watumishi wa serikali.

“Tunawachunguza watu 134 kuhusu ugonjwa wa Corona ambao wengi wao ni wale waliorudi nchini ikiwemo watumishi wa serikali kujua kama wapo salama na ugonjwa huo,” amesema.

Aidha, amesema imegundulika kuwepo kwa baadhi ya maduka yakiuza vifaa feki kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa Corona vikiwemo vitakasa mikono ambavyo havina viwango.

“Lipo duka moja tumelikamata likiuza vifaa vya kujikinga na corona ambavyo vinatengenezwa kienyeji...tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi wa tukio hilo,” amesema.

Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ikiwemo kuwabaini watu wanaoingia nchini kwa njia mbalimbali na kutoa taarifa haraka kwa vyombo husika.

KIWANGO cha mimba za utotoni kimeripotiwa kupungua kwa kasi katika ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi