loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Guardiola achangia bil 2/- kukabili corona

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amechangia kiasi cha pauni 920,000 (ambazo ni sawa na Sh bilioni 2.5 za Tanzania) kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona nchini Hispania.

Guardiola, ambaye kwa sasa yuko nyumbani kwao jijini Barcelona, kwa siku kadhaa sasa amekuwa akifanya kazi na wanasheria wake ili kuangalia njia nzuri zaidi ya jinsi ya kutumia fedha hizo.

Zitakwenda katika kampeni ya kupambana na vita ya kuzuia corona inayofanywa na Chuo cha Madawa cha Barcelona na Taasisi ya Misaada ya Angel Soler Daniel.

Hispania ni moja ya nchi iliyoathirika vibaya na mashambulizi ya virusi vya corona barani Ulaya.

Takwimu rasmi za juzi Jumanne zinaonesha kuwa watu 2,696 wamekufa nchi humo huku 40,000 wakiwa wameathirika na virusi hivyo.

Pia fedha hizo zitatumika kusaidia kununua vifaa tiba na vile va kujikinga kwa ajili ya wafanyakazi wa hospitali ambao wanahusuika na kutoa huduma za matibabu kwa wale waliolazwa.

Mkoa wa Catalan ni mmoja ya eneo lililoathirika zaidi na virusi vya corona nchini Hispania, ambalo lina wagonjwa wengi wa ugonjwa huo.

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wote wameripotiwa kuchangisha kiasi cha Euro milioni 1 katika kampeni za kupiga vita virusi vya corona wiki hii.

Gazeti la Michezo la Mundo Deportivo liliripoti kuwa Messi, ambaye ni mshambuliaji wa Barcelona alichangia kiasi cha Euro milioni 1 kwa hospitali mbili, moja iliyopo Barcelona na nyigine nchini kwao Argentina.

Ronaldo anayeichezea klabu ya Juventus ya Italia na timu ya taifa ya Ureno pamoja na wakala wake, Jorge Mendes amechangia kiasi cha Euro milioni 1 katika vyumba vitatu vya wagonjwa mahututi waliolazwa sababu ya corona huko Lisbon na Porto.

Wiki iliyopita, mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski alichangia kiasi cha Euro milioni 1 kwa ajili ya kupambana na virusi hivyo vya corona nchini Ujerumani.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi