loader
Picha

Wazazi wahatarisha maisha ya watoto

BAADHI ya watoto wenye umri tofauti hadi miaka minane, wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na wazazi kutumia vibaya likizo iliyotolewa na serikali.

Baadhi ya watoto hao wanapelekwa katika misongamano ya watu maeneo ya masoko na sehemu za biashara. Wengine wamepelekwa kwa bibi au babu zao wenye umri mkubwa.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitangaza kufungwa kwa siku 30 kwa shule zote na vyuo vyote, baada ya kuibuka nchini kwa ugonjwa wa homa ya mapafu, inayotokana na virusi vya corona.

Mwenyekiti wa Soko Kuu mjini Moshi, Badru Hassan alikiri kuwepo watoto katika soko hilo.

Alisema tahadhari zinaendelea kuchukuliwa, ikiwamo kunawa mikono na watoto kuachwa maeneo salama hususani nyumbani.

Hassan alisema hayo wakati akizungumzia utafiti wa kuongeza uelewa, uwajibikaji wa huduma bora za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto, unaotekelezwa na Muungano wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC) kwa kushirikiana na taasisi ya CiC ya Ireland.

“Ni kweli watoto wapo katika masoko na hakuna usalama wa kutosha, mtu anaweza kuwa na watoto wawili, yeye ndiye baba ndiye mama, tunatoa matangazo ya mara kwa mara kwa wateja na wafanyabiashara kufuata tahadhari zilizowekwa na serikali,” alisema.

Mmoja wa wakazi wa Kata ya Bondeni Manispaa ya Moshi, Faely Jumanne alisema ameshindwa kuwapeleka watoto wake kwa bibi yao kutokana na hofu ya kukosa uangalizi wa kutosha.

Kuhusu suala la usalama wa watoto ndani ya jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi 2019/2020, alisema watoto wameendelea kupata huduma za msingi.

Alisema katika kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019, watoto 13,420 walipatiwa huduma za msingi katika makao ya watoto ikilinganishwa na watoto 6,132 waliokuwa kwenye makao kwa mwaka 2017/18.

Aidha, Ummy alisema wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (Tamisemi) imetambua na kuwezesha huduma za msingi kwa watoto wanaoishi mitaani. Watoto 1,481,771 huku 930 kati yao waliunganishwa na familia zao.

KIWANGO cha mimba za utotoni kimeripotiwa kupungua kwa kasi katika ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Moshi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi