loader
Picha

Mil 76.6/-, nguvu wananchi vyatoa madarasa 5, ofisi 2

WANANCHI wa Kijiji cha Lindi Kata ya Lumecha Wilaya ya Nyasa kwa kushirikiana na serikali, wamejenga vyumba vitano vya madarasa, ofisi mbili za walimu na matundu sita ya vyoo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lindi, Kassian Komba amesema Serikali ilitoa Sh milioni 76.6 kutoka katika mradi wa Lipa Kutokana na Matokeo (P4R) kwa maelekezo kuwa Sh milioni 30 zitumike kujenga jengo la utawala, milioni 40 vyumba viwili vya madarasa na Sh milioni 6.6 kujenga matundu ya vyoo.

Wakazi wa kiijiji hicho katika kuiunga mkono serikali, wamejitolea nguvu zao kwa kufyatua matofali, kuchimba msingi na kusaidia kazi.

Fedha zilizotengwa kwa ajili ya madarasa mawili, ziliwezesha kuongeza madarasa mengine matatu. Komba alisema kutokana na ushirikiano huo wa wananchi, wamemaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa, hivyo kuwawezesha wanafunzi zaidi 400 kukaa kwa nafasi darasani.

Anasema sasa wanatarajia ufaulu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka huu, utaongezeka. Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Ogani Ndimbo aliishukuru serikali kwa kuwajengea vyumba vya madarasa.

Aliahidi watasoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya kitaifa. Mkazi wa kijiji hicho, Isidori Kilongosi alisema walifyatua matofali 70,000 ambayo yalitosha kujenga madarasa mawili na ofisi moja ya walimu.

Kaimu Ofisa Elimu ya Msingi wa Wilaya ya Nyasa, Oscar Elias alisema fedha zilizoletwa katika shule hiyo, zililenga kujenga vymba viwili vya madarasa, matundu sita ya vyoo.

Lakini kwa sababu miradi ya P4R inashirikisha wananchi wa maeneo husika, wazazi na wanakijiji hao walitumia fedha hizo kujenga vyumba vingine vitatu vya madarasa na ofisi moja ya walimu.

Elias alisema kumekuwa na matumizi mazuri ya fedha katika shule hiyo, ikilinganisha na maeneo mengine, kwani vyumba vitatu vilitakiwa kutumia milioni 60, badala ya Sh milioni 30.

KIWANGO cha mimba za utotoni kimeripotiwa kupungua kwa kasi katika ...

foto
Mwandishi: Amri Mmanja, Nyasa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi