loader
Picha

Wananchi Rukwa wakosa vipimo x-ray

BAADHI ya vipimo havifanyiki katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Rukwa, kutokana na mashine ya x-ray ambayo imetumika kwa zaidi ya miaka 30 kuchakaa.

Pia, ukarabati wa x-ray hiyo umeshindikana kutokana na kutopatikana kwa vipuri vyake. Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga, Dk John Lawi.

Gazeti hili lilimhoji Dk Lawi kuhusu malalamiko ya wananchi kuwa hospitali hiyo haina x-ray kwa zaidi ya miaka miwili.

“Si kweli ingekuwa hivyo tungebandika matangazo kuwataarifu wananchi, ukweli wake x- ray ipo, ila changamoto iliyopo ni miongoni mwa zile za zamani, imechakaa baada ya kutumika kwa zaidi ya miaka 30 sasa, hivyo baadhi ya vipimo havifanyiki kulingana na uchakavu wake... pia vipuri vyake havipatikani,” alisema.

Alisema, “katika hospitali zote za mikoa nchini, sisi ndio tumebaki nayo, ni aina ya Philips, hata upatikanaji wa vipuri vyake ni changamoto,” alifafanua.

Alisema wamekuwa wanawaelekeza wagonjwa wapate baadhi ya vipimo katika Kituo cha Afya Mazwi, ambacho kina x-ray mpya.

“Pia tunawaeleza waende kupata vipimo vya x-ray katika Hospitali Teule ya Dk Atman iliyopo eneo la Kristu Mfalme Manispaa ya Sumbawanga,” alieleza.

Aliongeza kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imebaini changamoto hiyo, ambapo imeahidi kuipatia hospitali hiyo x-ray mpya hivi karibuni.

Kuhusu malalamiko ya upungufu wa dawa, amesema “Upatikanaji wa dawa umegawanywa katika makundi kulingana na hadhi ya vituo vinavyotoa huduma za afya. Kutokana na hadhi ya hospitali yetu haturuhusiwi kuwa nazo, mgawanyo huo ni kulingana na hadhi ya zahanati, hospitali za wilaya, Kanda na Hospitali za mabingwa”.

Alisema upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo, bado ni wa chini ambao ni wastani wa asilimia 70, ila jitihada zinafanyika.

MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi