loader
Picha

Washitakiwa kesi ya rushwa Arusha kusomewa maelezo

MFANYABIASHARA maarufu jijini Arusha, Shabiby Virjee (34) na wenzake wawili akiwemo askari polisi anayekabiliwa na kesi ya rushwa ya Sh milioni 10, inaanza kusikilizwa leo jijini humo.

Kesi hiyo awali ilikuwa ianze kusikilizwa Februari 8 mwaka huu kwa watuhumiwa kusomewa maelezo ya awali lakini, ilishindikana kusikilizwa baada wakili wa mshitakiwa wa kwanza, Gwakisa Sambo kushindwa kufika mahakamani hapo na kuomba kuahirishwa kesi hadi leo.

Awali kesi hiyo ilikuwa ianze kusikilizwa Februari 8 mwaka huu, lakini Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Arusha, Martha Mahumbuga alikuwa safarini kikazi.

Kesi hiyo iliahirishwa mbele ya Hakimu Mkadhi, Nestory Baro hadi leo, na sasa washitakiwa wataanza kusomewa maelezo ya awali katika mahakama hiyo.

Waendesha mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Arusha (Takukuru), tayari wamekamilisha upelelezi wa kesi hiyo, hivyo wako tayari kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Hayo yalisemwa na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Hamidu Singano akiwa na Richard Jacopiyo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Arusha, Mahumbuga.

Mbali ya Virjee, wengine walioshitakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na aliyekuwa askari polisi Kituo Kikuu cha polisi Arusha, Paulo Erasmo (37) na mfanyakazi wa kampuni hiyo ya mafuta ya Oryx, Nkenzi Pazi (38).

Mfanyabiashara huyo na wenzake wanaotetewa na wakili Godluck Maico na Sambo Gwakisa, wanakabiliwa na mashitaka ya kutoa rushwa ya Sh milioni 10 ili kumpatia askari polisi, Meshack Laizer aliyekuwa amewakamata wafanyakazi wawili wa kampuni ya mafuta ya Oryx, wakiuza mafuta uchochoroni kinyume cha sheria.

KIWANGO cha mimba za utotoni kimeripotiwa kupungua kwa kasi katika ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi