loader
Picha

TPB yatoa saruji kujenga madarasa Rukwa

BENKI ya TPB imetoa mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya Sh milioni 3.6 ili kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati mkoani Rukwa.

Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakangata (CCM) aliomba msaada huo kupitia Serikali ya mkoa wa Rukwa.

Mkurugenzi wa Idara ya Tehama na Uendeshaji wa Benki ya TPB, Jema Msuya amesema msaada huo ni utekelezaji wa sera yao ya kushirikiana na jamii kuiwezesha sehemu yake ya faida.

"Majukumu yetu ni pamoja na kushirikiana na jamii inayotuzunguka kutatua changamoto zinazoikabili katika sekta ya elimu na afya kwa ustawi wa jamii,"alieleza.

Akipokea misaada huo, Mwakangata aliipongeza benki hiyo kwa utayari wake wa kutoa msaada huo. Alisema umetolewa katika muda mwafaka.

Alisema mifuko hiyo ya saruji, itasambazwa katika maeneo yenye mahitaji makubwa ili kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati.

"Kuna upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa unaozikabili shule zetu mkoani hapa, hii ni kutokana na idadi kubwa ya watoto wanaojiandikisha kila mwaka baada ya serikali kuanzisha mpango wa elimu bure,"alieleza.

Akitoa shukrani za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa, Reiner Lukala alisema mwaka jana benki hiyo ilitoa mifuko 200 ya saruji iliyosaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

KIWANGO cha mimba za utotoni kimeripotiwa kupungua kwa kasi katika ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi